Radio Fadhila

Upendo Charity wamfariji Bibi Sabra

8 August 2023, 11:16 AM

Wanakikundi  wa  Upendo Charity, kinachopatikana katika halamshauri ya Mji wa Masasi mkoani Mtwara, wameshiriki kufanya matendo ya huruma kwa kutoa maziwa ya Lactojeni dazeni moja na nguo za kujikinga na baridi kwa mtoto Sabra  aliyezaliwa hivi karibuni katika Hospitali ya Mkomahindo wilaya ya Masasi mkoani Mtwara na kumpoteza mama yake mzazi  kwa kufariki hivyo kupelekea mtoto huyo kulelewa na bibi yake anayefahamika kwa jina la Mwajuma Hassani Mkota au Bibi Sabra.

Mwenyekiti wa kikundi cha Upendo charity wa kwanza kushoto akiwa na wanakikundi wenzake katika picha ya kukabidhi mahitaji ya mtoto Sabra..

Akizungumza katika tendo hilo la kukabidhi mahitaji hayo mwenyekiti wa kikundi hicho Christine Simo akawa na haya ya kusema…

Sauti ya Christine Simo

Kwa upande wake diwani wa kata  ya Mkomahindo kilipotokea kisa hicho Ally Salvatori akizungumza katika  eneo la tukio pamoja na kuzungumza mengi juu ya faraja waliyotoa kikundi hicho kwa familia ya Bibi Sabra  akasema…

Sauti ya Ally Salvatori

Kwa upande wake Bibi Sabra akizungumza katika kutoa shukrani zake aliwashukuru wanakikundi hao kwa moyo wa upendo na ukarimu na kumwomba Mungu awazidishie zaid pale walipotoa wanakikundi hao.