Radio Fadhila

Mnada wa 6 wa zao la Korosho MAMCU LTD bei yapanda  

16 November 2026, 16:08 pm

Chama Kikuu cha Ushirika cha MAMCU LTD kimefanikiwa kuuza tani 7,076 za korosho katika mnada wa sita wa msimu wa 2026/2027 uliofanyika leo, Novemba 16, 2026, katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Masasi. Katika mnada huo, bei ya juu ya korosho imefikia shilingi 3,600 huku bei ya chini ikiwa shilingi 3,180 kwa kilo

Na Godbless Lucius

Chama Kikuu cha Ushirika cha MAMCU LTD kimefanikiwa kuuza jumla ya tani 7,076 katika mnada wake wa 6 wa zao hilo kwa msimu wa 2026/2027.

Mnada huo uliofanyika Katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji masasi leo Tarehe 16, Novemba 2026 bei ya juu imefikia shilingi 3,600 na bei ya chini ya shilingi 3,180 kwa kilo.