Radio Fadhila
Radio Fadhila
9 November 2026, 19:59 pm

Mnada wa 5 wa zao la korosho msimu wa 2026/2027 kupitia Chama Kikuu cha Ushirika cha MAMCU Limited umefanyika Novemba 9, 2026, katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Masasi, mkoani Mtwara huku bei ya zao hilo ikizidi kupanda na kufikia tsh 3,510.
Na Godbless lucius
nada wa tano wa korosho ghafi kwa msimu wa 2026/2027 kupitia Chama Kikuu cha Ushirika cha MAMCU Limited umefanyika Novemba 9, 2026, katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Masasi, mkoani Mtwara. Katika mnada huo, bei ya juu imefikia Sh 3,510 na bei ya chini Sh 3,260 kwa kilo.
Akizungumza kuhusu mwenendo wa malipo, Mwenyekiti wa MAMCU Limited, Alhaj Azam Mfaume Julajula, amesema malipo kwa wakulima yanaendelea vizuri, huku akiwataka wakulima ambao bado hawajalipwa kutoa taarifa kupitia namba maalumu iliyotengwa kwa ajili ya kupokea taarifa hizo ili hatua zichukuliwe.
Kwa upande wake, Mrajisi Msaidizi wa Mkoa wa Mtwara, Robert Nsunza, amewahimiza wanunuzi kuendelea kujitokeza kwenye minada, akieleza kuwa bado kuna korosho za kutosha. Aidha, amewataka wanunuzi kulipa kwa wakati ili kuwawezesha vyama vya ushirika kuwalipa wakulima kwa wakati na kuimarisha ufanisi wa mfumo mzima wa ununuzi wa korosho.
Sauti ya Mkiti wa Mamcu na Mrajis Msaidizi