Radio Fadhila

Safari ya Eva Mabula katika kilimo cha mbogamboga-Makala

26 September 2026, 07:09 am

Makala hii inamuelezea Eva Mabula mwanamke aliyeanzisha kilimo cha mbogamboga kwa ajili ya kuikomboa familia yake mpk sasa kilimo hicho kimekua chanzo kikubwa cha mapato.

Eva Mabula, mama mwenye umri wa miaka 40 na watoto watano, amekuwa akijishughulisha na kilimo cha mbogamboga kwa miaka 16. Alianza kilimo hicho kutokana na hali ngumu ya maisha, akilenga kupata kipato cha kugharamia mahitaji ya familia yake na kuhakikisha watoto wake wanapata mahitaji muhimu.

Mpaka sasa kilimo cha mbogamboga kimekuwa na mafanikio kwake. Kwa mfano, kwa siku moja kupitia mchicha pekee, Eva anaweza kupata kipato cha hadi shilingi elfu 80,000, huku akiwa mpaka sasa ameweza kutoa ajira kwa zaidi ya wafanyakazi 10.

Makala ikisomwa na Edwin Mpokasye