Radio Fadhila
Radio Fadhila
27 September 2026, 17:52 pm

Baada ya kufanya ziara na kusikiliza changamoto za wanafunzi wenye mahitaji maalum shele ya Msingi Masasi Hatimae Mbunge Viti maalum Mtwara Mh, Asha Motto ametekeleza ahadi yake Septemba 26,2026.
Na Godbless Lucius
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mtwara, Asha Motto, ametimiza ahadi yake ya kuwapatia viti mwendo vinne (4) wanafunzi wenye mahitaji maalum katika Shule ya Msingi Jumuishi Masasi, ikiwa ni hatua ya kuwasaidia kupata unafuu na kushiriki kwa urahisi zaidi katika shughuli zao za masomo.
Motto amesema utekelezaji wa ahadi hiyo umetokana na ziara aliyowahi kufanya shuleni hapo, ambapo alielezwa changamoto zinazowakabili wanafunzi wenye mahitaji maalum, ikiwemo ukosefu wa viti mwendo, fimbo za kuwaongoza njia pamoja na baadhi ya vitendea kazi kwa wanafunzi wenye uoni hafifu wanaosoma kwa njia ya Nukta Nundu (Braille), ikiwemo karatasi maalum za Lime Paper.
Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Rachel Kassanda, amempongeza Mbunge huyo kwa mchango huo, akieleza kuwa umefika moja kwa moja kwa watu wenye uhitaji
https://www.instagram.com/p/Ddy10JjjNKP/?utm_source=ig_web_copy_link&stkn=MzRlODBiNWFlZA==