Radio Fadhila
Radio Fadhila
20 October 2026, 11:25 am

Mwenyekiti wa Bodi ya MAMCU LTD, Alhaj Azam Mfaume Julajula, amesema mnada wa pili wa korosho msimu wa 2026/2027 umefanyika kwa mafanikio Nanyumbu, Mtwara, ambapo bei ya juu imefika Sh 3,360 na ya chini Sh 3,130 kwa kilo. Amesema tani 18,689 zimeuzwa katika mnada huo, na kufanya jumla ya tani 30,274 kuuzwa kupitia minada miwili, zenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 98
Na Godbless Lucius
Chama Kikuu cha Ushirika cha MAMCU LTD kimefanikiwa kufanya mnada wa pili wa korosho kwa msimu wa 2026/2027, uliofanyika Jumatatu, Oktoba 19, 2026, katika Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara, ambapo jumla ya tani 18,689.554 za korosho zimeuzwa.
Akizungumzia matokeo ya mnada huo, Mwenyekiti wa Bodi ya MAMCU LTD, Alhaj Azam Mfaume Julajula, amesema mnada huo umefanyika kwa mafanikio kupitia mfumo wa Soko la Bidhaa Tanzania (TMX), huku bei ya juu ya korosho ikifikia Shilingi 3,360 kwa kilo na bei ya chini ikiwa Shilingi 3,130 kwa kilo.
Alhaj Julajula amesema kuwa baada ya kukamilika kwa minada miwili ya mwanzo, MAMCU LTD imefanikiwa kuuza jumla ya tani 30,274 za korosho zenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 98, hali inayoonesha mwenendo mzuri wa biashara ya korosho katika msimu huu.
sauti ya viongozi wa mamcu