Radio Fadhila
Radio Fadhila
22 September 2026, 18:45 pm

Na Godbless Lucius
Watu wenye ulemavu katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi wamehimizwa kutumia fursa ya mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Serikali ili kujikwamua kiuchumi. Kati ya fedha hizo, asilimia 2 imetengwa kwa ajili ya watu wenye ulemavu.
Watu wenye ulemavu katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi wamehimizwa kuchangamkia fursa ya mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Serikali kwa lengo la kuwawezesha kujikwamua kiuchumi kupitia shughuli mbalimbali za uzalishaji.
Kwa mujibu wa Afisa Maendeleo na Mratibu wa Watu Wenye Ulemavu katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, Sospeter Lucas Nyagalu, asilimia 2 ya mikopo hiyo imetengwa kwa ajili ya makundi ya watu wenye ulemavu, hivyo amewataka walengwa kutumia fursa hiyo kuanzisha na kuendeleza shughuli za kiuchumi.
Sauti ya Mratibu wa Watu Wenye Ulemavu Sospeter Lucas Nyagalu