Radio Fadhila

Polisi Masasi wawafikia wenye mahitaji maalum shule ya Lukuledi

14 September 2026, 12:10 pm

picha ya pamoja polisi na wanafunzi

Picha na Godbless lucius

Miongoni mwa watu wanaohitaji faraja ya karibu ni watu wenye mahitaji maalumu, hivyo jeshi la Polisi kwa kulijua hilo nimeamua kuwatembelea wanafunzi wenye mahitaji katika shule ya Lukuledi ili kufurahi nao pamoja.

Wanafunzi wenye mahitaji maalum wa Shule ya Msingi Lukuledi Maalum wilayani Masasi, mkoani Mtwara, wamewashukuru askari wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Masasi kwa kuwafanyia ziara ya kuwafariji, kuwapa zawadi na kuwahamasisha katika safari yao ya elimu.

Ziara hiyo imeongozwa na OCS wa Polisi Wilaya ya Masasi, Sadick Kajosi, ambapo askari hao walizungumza na wanafunzi na kuwahimiza kuendelea kusoma kwa bidii, kujiamini na kutokuruhusu mahitaji maalum kuwa kikwazo cha kufikia ndoto zao.

Sauti ya OCS Sadick Kajosi

Katika ziara hiyo, Jeshi la Polisi lilitoa zawadi mbalimbali zikiwemo sabuni za kuogea na kufulia, taulo za watoto wa kike pamoja na vinywaji. Uongozi wa shule pamoja na wanafunzi umeeleza kuwa ziara hiyo imewapa faraja na hamasa ya kuendelea na masomo.