Radio Fadhila
Radio Fadhila
4 September 2026, 13:53 pm

Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira na Wanyamapori (WWF Tanzania) limeendelea kuwawezesha vijana katika Halmashauri ya Mji Masasi kushiriki kikamilifu katika utunzaji wa mazingira kupitia programu ya Youth Grassroot Leadership, inayolenga kuwajengea uwezo vijana kutambua na kutatua changamoto za kimazingira zinazoikabili jamii.
Na kwaupande wake afsa Afya ndg Emannuel mbogo aliosema kuwa anashukuru sana wadau waliojitokeza kuungana na kufanikisha zoezi la usafi wa mazingira
Afisa Habari na Mawasiliano wa WWF Tanzania, Bw. Japhary Kiwanga, amesema programu hiyo inalenga kuwaweka vijana mstari wa mbele katika masuala ya uhifadhi wa mazingira, pamoja na kuwashirikisha katika utoaji wa elimu kwa jamii na wanafunzi walioko shuleni.
Amesema kupitia ushirikiano kati ya WWF Tanzania na Halmashauri ya Mji Masasi, vijana wameendelea kushiriki katika shughuli mbalimbali za kimazingira, ikiwemo zoezi la usafi lililohusisha ukusanyaji wa taka katika maeneo mbalimbali na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu namna bora ya kudhibiti taka zinazozalishwa katika maeneo ya makazi na biashara.
