Radio Fadhila

Askofu Almasi: Tumemuona Mungu akitupigania kwa miaka 100

23 September 2026, 14:19 pm

Picha ya kanisa la Anglikana Dayosisi ya Masasi imepigwa na Edwin Mpokasye

Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Masasi linasherekea maadhimisho ya Jubilei ya miaka 100Askofu Almasi amesema katika safari ya miaka 100, Dayosisi imepitia “mawimbi” ya matatizo na dhiki, lakini Mungu ameendelea kuwa mshindi

Na Godbless Lucius

Askofu Dkt. James Almasi wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Masasi amewaalika waumini kuungana katika maadhimisho ya Jubilei ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Dayosisi hiyo.

Askofu Almasi amesema mwaka 2026 ni wa kihistoria kwa Dayosisi hiyo, huku akimshukuru Mungu kwa kuiwezesha kuvuka changamoto mbalimbali kwa kipindi cha miaka 100. “Mambo mengi yamepita, lakini tumemuona Mungu akitupigania na tukashinda,” amesema.

Amesema Dayosisi imepitia mawimbi ya matatizo na dhiki, lakini Mungu ameendelea kuwa mshindi. Ameongeza kuwa kufikia miaka 100 si kwa nguvu, ujanja wala maarifa ya binadamu, bali ni kwa msaada wa Mungu.