Radio Fadhila
Radio Fadhila
7 October 2026, 11:36 am

Na Godbless Lucius
Galantina Salvatory Mgongo kutoka Sekretarieti ya Kuzuia na Kupambana na Usafirishaji Haramu wa Binadamu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, amesema mitandao ya kijamii inaweza kuwa chanzo cha hatari kwa watu wanaovutiwa na maisha ya kifahari yanayoonyeshwa mtandaoni bila kuzingatia usalama wao.
Amesema pamoja na kuwa mitandao hiyo inaweza kutumiwa na wahalifu kuwavuta waathirika, pia imekuwa na mchango mkubwa katika kuwaokoa watu wanaofanyiwa usafirishaji haramu wa binadamu, kwa baadhi yao kutumia mitandao hiyo kuomba msaada wanapokwama.
sauti ya Bi Galantina na Godbless katika kipindi