Radio Fadhila

Mtandao sababu ya mnada wa kwanza wa zao la Korosho kuendelea kufanyika 13,10,2026 MAMCU LTD

12 October 2026, 18:57 pm

Mnada wa kwanza wa korosho kwa msimu wa 2026/2027 kupitia Chama Kikuu cha Ushirika cha Mtwara Masasi (MAMCU LTD), uliokuwa ufanyike leo, Jumatatu, Oktoba 12, 2026, umeahirishwa hadi kesho, Jumanne, Oktoba 13, 2026, kutokana na changamoto za mtandao.

Na Godbless Lucius

Mnada wa kwanza wa korosho kwa msimu wa 2026/2027 kupitia Chama Kikuu cha Ushirika cha Mtwara Masasi (MAMCU LTD), uliokuwa ufanyike leo, Jumatatu, Oktoba 12, 2026, umeahirishwa hadi kesho, Jumanne, Oktoba 13, 2026, kutokana na changamoto za mtandao.Mnada huo ulianza vizuri, lakini shughuli za uuzaji hazikuweza kuendelea kama ilivyopangwa baada ya kukabiliwa na hitilafu za mtandao.

Akizungumza kuhusu kuahirishwa kwa mnada huo, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Francis Alfred, amesema kuwa kati ya loti 64 zilizokuwa zimepangwa kuuzwa, ni loti 5 pekee zilizofanikiwa kuuzwa kabla ya changamoto hiyo kujitokeza. Ameeleza kuwa bei ya chini ya korosho iliyouzwa ilikuwa shilingi 3,040 kwa kilo, huku bei ya juu ikiwa shilingi 3,310 kwa kilo

Sauti ya Mkurugenzi wa (CBT), Francis Alfred

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya MAMCU LTD, Alhaj Azam Mfaume Julajula, ametangaza kuwa mnada huo utaendelea kesho, Jumanne, Oktoba 13, 2026, katika Ukumbi wa Masasi Mji, kuanzia saa 4:00 asubuhi. Hatua hiyo inalenga kutoa nafasi ya kukamilisha shughuli za mnada zilizoshindwa kuendelea leo kutokana na changamoto za mtandao