Radio Fadhila

Mradi wa maji wawaondolea wananchi hofu ya Mamba Nanyumbu

25 September 2026, 11:40 am

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) ametembelea mradi Maji wa Masuguru na kuridhishwa na kazi iliyofanyika.(Na Mpiga picha wetu)

Mradi mkubwa wa maji wa miji 28 unaotekelezwa katika kijiji cha Masuguru,wilaya ya Nanyumbu, mkoani Mtwara umeleta mabadiliko makubwa katika maisha ya kila siku ya wananchi.

Na mwandishi wetu

Akizungumza na wananchi wa Nanyumbu katika mkutano wa hadhara amesema mradi huo ni moja ya ahadi ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambayo ameikamilisha.

Mradi wa maji wa miji 28 wenye thamani ya shilingi Bilioni 38 na uwezo wa kuzalisha Lita milioni 5 kwa siku utekelezaji ukiwa asilimia 97 umeanza kutoa huduma kwa wananchi takriban elfu 81.

Mradi huo unatarajiwa kuhudumia pia wakazi wa Masasi, Nachingwea na baadhi ya vijiji vya wilaya ya Ruangwa.

Sauti ya Waziri wa Maji Juma Aweso