Radio Fadhila

Mshana atoa wito wazazi kuwekeza kwenye elimu

14 November 2026, 14:34 pm

Katika mahafali ya tatu ya Shule ya Sekondari Sengenya, yaliyohitimishwa na takribani wanafunzi 30, mgeni rasmi Halfan Mshana, Mkuu wa Chuo cha Masasi FDC, amesisitiza umuhimu wa kuwekeza katika elimu akisema, “Tunapowekeza kwenye elimu huwa hatupotezi bali tunakopesha.” Amewataka wahitimu kuzingatia nidhamu, bidii na maadili mema, huku akiahidi kusaidia upatikanaji wa magoli ya chuma, mipira na betri ya sola ili kuboresha mazingira ya shule.

Na Godbless Lucius

hule ya Sekondari Sengenya imefanya mahafali yake ya tatu, ambapo takribani wanafunzi 30 wamehitimu elimu ya sekondari. Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa shule ameeleza kuwa licha ya changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo, mahitaji makubwa kwa sasa ni upatikanaji wa betri ya sola pamoja na magoli ya chuma kwa ajili ya kuimarisha shughuli za michezo shuleni hapo.

Akizungumza katika maafali hayo Mgeni rasmi, Mkuu wa Chuo cha Masasi FDC, Halfan Mshana, amesema uwekezaji katika elimu ni uwekezaji wenye faida kubwa kwa mtu binafsi na taifa. Amesema, *“Tunapowekeza kwenye elimu huwa hatupotezi bali tunakopesha, na hakuna biashara nzuri duniani kama kuwekeza kwenye elimu.” Aidha, amesisitiza kuwa hakuna mtoto wa familia maskini anayeshindwa kuwa kiongozi mkubwa ikiwa wazazi na walezi watawekeza katika elimu yake.

sauti ya Mshana

Mshana amewataka wahitimu kutokutegemea vyeti pekee kama njia ya mafanikio, bali kuzingatia nidhamu, utii, bidii, maadili mema na hofu ya Mungu. Amesema, “Kupata cheti tu si njia ya mafanikio; mafanikio yanaongozwa na nidhamu, utii, bidii na maadili mema. Tunahitaji wasomi wenye maadili, nidhamu na hofu ya Mungu.”

Katika hatua nyingine, mgeni rasmi huyo ameahidi kushughulikia changamoto zilizowasilishwa na mkuu wa shule, akisema kuwa kabla ya shule kufunguliwa mwaka 2027, magoli ya chuma yatakuwa yamepatikana. Pia ameahidi kutoa mipira kwa ajili ya michezo na kuomba apewe taarifa za ukubwa na aina ya betri ya sola inayohitajika ili aweze kushughulikia upatikanaji wake