Radio Fadhila
Radio Fadhila
29 September 2026, 15:55 pm

Picha ya Mkiti wa UVCCM Masasi CDE Namtus
Baada ya madai ya kuwepo kwa mpango wa kumuondoa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi pamoja na madai ya baadhi ya Madiwani kugushiwa saini zao za kutokua na imani na mwenyekiti huyo CDE Namtus ameomba uchunguzi ufanyike huku akieleza Chama chao hakihusiki na mpango huo.
Na Godbless Lucius
Mwenyekiti wa UVCCM Masasi, Cde Abdul Seif Namtusi, amempongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kazi anayoendelea kufanya katika Wilaya ya Masasi, huku akieleza msimamo wa chama kuhusu tuhuma za mpango wa kumuondoa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, Mheshimiwa Bashiru Mboneche.
Akizungumza na waandishi wa habari Septemba 29, 2026, Namtusi amesema Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya ya Masasi haijawahi kujadili wala kuidhinisha mpango wa kumuondoa Mboneche.
“Suala hili na mpango huo uko nje kabisa na Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya ya Masasi. Hatujawahi kukaa wala kujadili mpango wa aina hiyo,” amesema Namtusi.
Sauti ya Mkiti namtus kuhusu akikanusha ccm kutohusika na mpango huo
Kuhusu madai ya baadhi ya madiwani kulazimishwa au kugushiwa saini kwenye nyaraka zinazohusiana na mchakato huo, Namtusi amezitaka TAKUKURU na Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini ukweli wa tuhuma hizo.
Sauti ya Mkiti Namtus kuhusu malalamiko ya baadhi ya madiwani