Orkonerei FM
Waandishi wa habari wametakiwa kutumia kalamu zao viziri
28 March 2022, 6:09 pm
Na pascal sulle Tanga
Waandishi wa habari kutoka redio za kijamii wametakiwa kutumia kalamu zao vizuri katika kuandika habari zinazozingatia maadili ya uandishi wa habari ndani ya jamii.
Akizungumza wakati akifungua semina ya waandishi wa habari iliyoandaliwa na tume ya taifa ya UNESCO TANZANIA Mkuu wa wilaya ya tanga mkoani tanga Hashim mgandilwa wakati akifungua mafunzo ya siku tatu ya waandishi wa habari yanayofanyika mjini Tanga yanayoelenga kuwambusha maadili ya uandishi wa habari na haki za binadamu.
Amesema kuwa waandishi wa habari ni kama viongozi ambao wanawajibu wa kuzifahamu changamoto na kutafuta ufumbuzi wenye lengo la kuleta maendeleo katika jamii na kwamba jamii ni lazima ielimishwe juu ya namna ya kupata habari.
Kwa upande wake Katibu mtendaji wa Tume ya taifa ya Unesco, Profesa KHAMIS MALEBO amewataka waandishi wa habari kuzingatia maadili ya kazi yao na kujiepusha na rushwa ili kuandika habari zenye ukweli pasipo na upendeleo wowote.
Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo, wameipongeza Tume ya taifa ya unesco kwa mafunzo hayo kwani yatawasaidia kuwakumbusha wajibu wa utendaji kazi za kila siku katika maeneo yao.