ZIARA YA KAMATI YA SIASA WILAYA YA KICHAMA MERU KUKAGUA UTEKELEZAJI WA MIRADI.
16 March 2022, 7:41 pm
HABARI ARUSHA.
Kamati ya Siasa Wilaya ya Kichama Meru imepongeza utekelezaji wa miradi yenye thamani ya Shilingi Milioni 470 inayoendelea katika Shule mpya ya Ambureni.
Akizungumza wakati wa Ziara Shuleni hapo Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM )Wilaya ya kichama Meru Ndg.Gurisha Mfanga ambaye amemwakilisha Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya hiyo, amewapongeza utekelezaji wa miradi inayoendelea katika Shule mpya ya Sekondari Ambureni na kuelekeza Viongozi kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati na Watoto wa kitanzania wanaendelea kunufaika kwa kupata Elimu Bora Katika umbali mdogo ikizingatia Kata ya Ambureni ilikuwa haina Shule ya Sekondari .
Aidha Gurisha amepongeza ushirikiano uliopo kwa Viongozi wa Wilaya hiyo , Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru na Mkurugenzi Mtendaji sambamba na Mhe.Diwani , Mwenyekiti wa kijiji na Wananchi wa Kata ya Ambureni ambapo amehimiza Viongozi kuendelea kushirikiana na kuhakikisha mahitaji na vifaa vinapatikana kwa wakati ili Mradi usikwame”katika Kutekeleza miradi hii mkikwama toeni taarifa hatuta sita Kushuka kwani Serikali na Chama kipo kuwasaidia”amesema Gurisha
Wajumbe wengine wa Kamati hiyo wameshauri kutokana na ukubwa wa Miradi inayoendelea usimamizi uongezwe ili Miradi ikamilike kwa wakati na kwa tija iliokusudiwa”tunaomba Mkurugenzi ahakikishe kunakuwa na usimamizi wa kutosha kwenye Mradi huu”amesema Joshua Mbwana ambaye ni katibu mwenezi wa CCM Wilaya hiyo
Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya ameendelea kuishukuru Serikali kutoa fedha za maendeleo ambapo imetoa Shilingi Milioni 470 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali katika Shule hiyo mpya ya Ambureni, Pia ilitoa Milioni 80 kwa ajili ya ujenzi wa Vyumba viwili vya Madarasa vilivyokamilika.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe.Mhandisi Richard Ruyango amesema Wilaya hiyo inaendelea Kutekeleza Ilani ya CCM kwa kuhakikisha miradi inatekelezeka kama ilivyokusudiwa ambapo ameelekeza Halmashauri kuhakikisha mafundi wanafanya Kazi kwa muda iliokusudiwa.
Nao Wananchi wa Kata ya Ambureni wameishikuru Serikali ya Awamu ya Sita ikiongozwa na Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa Shule Mpya ya Ambureni “Tunamshukuru Mhe.Rais kwa kipindi kifupi tumeletewa hela nyingi watoto wetu watatembea umbali mdogo ” amesema Erasto Mkazi wa Ambureni
“Sisi Viongozi wa Kiserikali tunaushirikiano mzuri na tunaahidi kuendelea kushirikiana kuwaletea Wananchi maendeleo”amesema Mhe.Faraja Diwani wa Kata ya Ambureni
Aidha ziara hiyo ya Kamati ya Siasa umekamilika kwa Siku ya kwanza ambapo wajumbe wamekagua miradi inayoendelea kwenye Shule mpya ya Ambureni itakayo gharimu Milioni 470 ,Mradi wa maabara za biolojia na chemistry zenye thamani ya million mia Moja katika Shule ya Sekondari Patandi Maalum na ujenzi wa Nyumba ya Mtumishi (2 in One ) ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa dharura (EMD) katika Hospitali ya Wilaya litakalo gharimu Milioni 300 na ujenzi wa chumba Cha darasa katika Shule ya Sekondari Seela.