On air
Play internet radio

Recent posts

8 October 2024, 4:40 pm

Mpango mkakati wa miaka 5 uendane na uimarishaji huduma bora kwa jamii

Na Mary Julius. Mkuu wa Mkoa Kusini Unguja  Ayoub Mohd Mahmoud, amewataka  viongozi na watendaji  wa baraza la mji kati Kuhakikisha  mpango mkakati wa miaka mitano wanao uandaa unalenga uimarishaji wa huduma  Bora  kwa jamii na unakidhi  mahitaji  ya wananchi.…

8 October 2024, 2:26 pm

UWT Zanzibar watakiwa kujiandikisha daftari la kudumu la mpiga kura

Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Magharibi kichama Tauhida Galos Nyimbo amewataka Wanachama wa UWT kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la kudumu la wapiga kura linaloendelea. Tauhida ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kukaguwa zoezi la uandikishaji wa Daftari…

7 October 2024, 4:51 pm

Diwani Viti Maalum akagua miradi ya maendeleo Wilaya ya Kati

Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii Baraza la Mji Kati ambaye pia ni Diwani wa viti maalum Riziki Muhammed Abdalla amewataka Wanajamii kushirikiana pamoja kuitunza na kuimarisha Miradi ya maendeleo inayojengwa katika maeneo yao ili iweze kudumu. Riziki ameyasema…

3 October 2024, 5:29 pm

Saba mbaroni kwa kufanya mauaji Mkoa wa Mjini Magharib

Na Salhey Hamad Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi linawashikilia watuhumiwa 05 ambao wamehusika katika matukio mawili ya mauaji yaliyotokea huko Kisakasaka na Mombasa Kwamchina Wilaya ya Magharibi B, pia linaendelea na uchunguzi wa tukio la mauaji lililotokea Kijichi…

3 October 2024, 3:56 pm

Adhabu kali atakayetumia mifuko ya plastik Zanzibar

Na Khalida Abdulrahman na Jesca Pendael. Jamii visiwani Zanzibar imetakiwa kuacha kutumia mifuko ya plastik  ili kuepukana na uchafuzi wa mazingira, uharibifu wa ardhi pamoja na vifo vya wanyama kama ng’ombe na mbuzi. Akizungumza na Zenj FM, Afisa wa Mazingira Hamdu…

28 September 2024, 9:47 am

Askari wa KVZ aliyedaiwa kupotea apatikana akiwa amefariki

Na Omary Hassan Askari wa Kikosi cha Valantia (KVZ) SGT Haji Machano Mohamed ambaye inasemekana alipotea akiwa katika Mafunzo ya Uongozi (Afisa Cadet) tangu Agosti 8, 2024 ameonekana jana akiwa amefariki dunia. Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi…

26 September 2024, 3:45 pm

Bodi ya Mkonge kuboresha maisha ya wajasirimali Pemba

Na Mary Julius Mratibu wa Mradi wa Mkonge na Bidhaa Zitokanazo na Mkonge Zanzibar Joseph Andrew Gasper amesema Bodi ya Mkonge Tanzania  ina malengo ya kushirikiana na wajasirimali wa kisiwani Pemba ili kuona wajasiriamali wananufaika na fursa zitokanazo na mkonge.…

25 September 2024, 6:31 pm

Vijana jitokezeni kugombea nafasi za uongozi CUF Zanzibar

Na Khalida Abdulrahman Chama cha Wananchi CUF kimewataka vijana kujitokeza kwa wingi katika kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho. Akizungumza na Zenj FM Mkurugenzi wa Itifaki na Udhibiti wa Chama Cha Wananchi CUF Taifa Rajab Mbarouk Mohd akiwaa  makao…

25 September 2024, 4:22 pm

Bei ndogo ya mwani kilio kwa wakulima Pwani Mchangani

Na Mwanaisha Msuko. Wananchi wa Pwani Mchangani Mkoa wa Kaskazini, wilaya ya Kaskazini A Unguja wameiomba serikali kuongeza bei ya mwani ili kuweza kumkomboa mkulima wa zao hilo. Wakizungumza na Zenji FM wakulima hao wamesema bei ndogo ya mwani inarudisha…