Zenj FM

Walokosa kuingizwa kaya maskini watakiwa kukata rufaa.

17 November 2021, 1:45 pm

Mratibu wa kaya maskini Tasaf Makame Ali Haji akiwa na wanufaika na miradi ya tasaf

Na Mary Kitipwi:Mratibu wa mpango wa kunusuru kaya masikini unguja TASAF Makame Ali Haji amesema serikali ya mapinduzi imetoa nafasi kwa wale wote wenye sifa za kuingizwa katika maradi wa kaya maskini ambao majina ya yamekatwa katika awamu ya kwanza kujaza form ambazo zinapatikana kwa masheha wa shehia zao.

Akizungumza na zenj fm mratibu wa mpango wa kunusuru kaya masikini unguja Makame Ali Haji hizo amesema maafisa wa tasaf watapitia upya fomu hizo na  kuwahakiki ili kuweza kuingizwa katika mpango huo.

Aidha mratibu amewaomba wabunge na wawakilishi kushirikiana katika kuwatambua na kuwaibua wale wanao hitaji kuingizwa katika mpango huo.