Karagwe FM

Katibu CCM Karagwe: Leeni watoto kimaadili

2 June 2023, 10:32 pm

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya Karagwe Bw. Anathory Nshange amewataka wazazi na walezi kulea watoto wao katika maadili ya kitanzania na kiimani

Bw. Nshange ameyasema hayo wakati akiongea kwenye mahafali ya tano ya chuo cha Karaduce wilayani Karagwe mkoa wa Kagera.

Nshange ametumia jukwaa hilo kuwataka wazazi na walezi kuwalea vyema watoto ili wajitenge na mambo maovu.

Nshange ameahidi kulea chuo hicho na kuhakikisha kinapata eneo kwa ajili ya ujenzi wa chuo ili kutimiza ndoto na malengo ya chuo hicho.

Kwa upande wake mkuu wa chuo hicho Mwl. Mugisha Thimotheo amewashukru wazazi kwa ushirikiano walioutoa kwa kipindi chote huku akiwasisitiza wahitimu kuendelea kujitolea kufanya kazi hata huko waendako kwa kuwa malengo ya chuo ni pamoja na kuendelea kutoa elimu ya maadili, itifaki, tehama na misingi bora ya utumishi.