Buha FM Radio

Wizi, kutoroka na kukataa shule, changamoto zinazoikabili kituo cha Center of Hope Kasulu.

30 October 2026, 12:16 pm

Mlezi wa watoto katika kituo cha Center of Hope Kasulu, mkoani Kigoma. Bi. Janet Josefu Nkamata. Picha na Emily Adam

Kituo cha Center of hope kinachojihusisha na malezi ya watoto waliotokea mazingira magumu kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na wizi, na baadhi ya watoto kutozoea kuishi katika mazingira hayo.

Na; Emily Adam.

Kituo cha Center of hope kinachojihusisha na malezi ya watoto waliotokea mazingira magumu, hatarishi na wenye ulemavu kilichopo halmashauri ya mji Kasulu mkoani Kigoma kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo baadhi ya watoto kuiba vitu na kutoroka kutokana na kutozoea kuishi kituo hapo.

Hayo yamebainishwa na mmoja wa walezi wa watoto katika kituo hicho Bi. Janet Josefu Nkamata wakati akizungumza na Buha FM Radio na kusema licha kituo hicho kutoa huduma ya afya, msaada wa kisheria pamoja na elimu kwa wahanga lakini bado kuna baadhi yao wanakataa kwenda shule kuanza masomo kutokana na umri pamoja na kutamani kurudi kuishi mtaani.

Sauti ya mlezi wa watoto katika kituo cha Center of Hope Kasulu, mkoani Kigoma. Bi. Janet Josefu Nkamata.

Aidha ameongeza kuwa kuna wakati kituo hicho hukumbwa na changamoto ya kupokea idadi kubwa ya watoto kuliko uwezo wake kutoka mtaani wakati kikiwa na uwezo wa kutunza na kuhudumia jumla ya watoto 45 pekee.

Sauti ya mlezi wa watoto katika kituo cha Center of Hope Kasulu, mkoani Kigoma. Bi. Janet Josefu Nkamata.
Baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo cha Center of Hope Kasulu, mkoani Kigoma. Picha na Emily Adam.

Hata hivyo Bi. Janeti ameishukuru serikali kwa ushirikiano mkubwa inaotoa kwa kituo cha Center of Hope katika swala la elimu, afya, chakula na misaada mbalimbali kwa watoto wanaolelewa kituoni hapo.

Sauti ya mlezi wa watoto katika kituo cha Center of Hope Kasulu, mkoani Kigoma. Bi. Janet Josefu Nkamata.

Kituo cha Center of Hope kwa sasa kina jumla ya watoto 36 ambapo kinatoa huduma mbalimbali kwa watoto hao ikiwemo elimu, afya, chakula, mavazi na malazi kwa watoto wanaotokea mazingira magumu, hatarishi na wenye ulemavu.