Buha FM Radio

Mradi wa maji wa miji 28 Kasulu wamkosha Mwang’onda

11 September 2026, 9:44 am

Mwaonekano wa mradi wa Maji wa Miji 28 katika Kata ya Msambala Halmashauri ya Maji Kasulu. Picha na Saharifat Shinji.

Katika kutekeleza kapeni ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kumtua mama ndoo kichwani, serikali ya Halmashauri ya Mji Kasulu imeendelea kutekeleza kwa ufanisi mradi wa maji wa Miji 28 ambao ushafikia hatua nzuri ya utekelezaji.

Na; Sharifat Shinji

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2026 Wazo Mwang’onda amefurahishwa na ujenzi wa  mradi wa  wa Maji wa Miji 28 katika Kata ya Msambala Halmashauri ya Mji Kasulu unaotekelezwa kwa fedha za Serikali kuu huku akisistiza mradi huo ukamilike  kwa wakati ili uwanufaishe wananchi.

Mwang’onda ametembelea  mradi huo na kukagua jinsi mradi huo unavyoendelea huku akisema ameridhishwa na utekelezaji wa mradi huo ambao hadi sasa umefikia zaidi ya asilimia 70 ya ujenzi huo na kuipongza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jinsi inavyoendelea kuwekeza katika miundombinu ya maji kwa Watanzania.

Sauti ya Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru 2026 Wazo Mwang’onda.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2026 akitoa maelekezo baada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa mradi wa Maji wa miji 28 uliopo kata ya Masambala Halmashauri ya Mji Kasulu. Picha na Sharifat Shinji.

Aidha Mwang’onda amewaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa serikali na kusema Serikali itaendelea kutekeleza miradi ya Maji ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma hiyo kwa wakati huku akiwataka viongozi kusimami na kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati.

Sauti ya Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru 2026 Wazo Mwang’onda.

Awali akisoma taarifa ya mradi huo Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji wilayani Kasulu Mhandisi Lucas Mgisha amesema mradi huo umeanza kutekelezwa Apr 11, 2023 na unatarajiwa kukamilika mnamo July 21, 2027 ukiwa uanagharimu zaidi ya bilioni 34 ambapo hadi bilioni 20.296 sawa na asilimia 58 zimeshalipwa kwa Mkandarasi na huo unatarajia kuwahudumia wananchi zaidi ya laki moja wa Halmahauri ya Mji Kasulu.

Sauti ya Mhandisi Lucas Mgisha.
Mkurugenzi wa Maji wa mamlaka ya Maji wilayani Kasulu akisoma taarifa ya utekelezaji wa Mradi. Picha na Sharifat Shinji.

Katika hatua nyingine Mbunge wa Jimbo la Kasulu Mjini Prof. Joyce Ndalichako amesema mradi huo utaenda kuatua changamoto ambayo imekuwepo kwa muda mrefu katika Halmashauri ya Mji Kasulu na ameongeza kuwa mradi utaweza kuzalisha lita milioni 15 hivyo amesema kutokana na pesa iliyotolewa na Serikali utaenda kuwa suluhisho kupitia mradi huo.

Sauti ya mbuge wa Jimbo la Kasulu Mjini Joyce Ndalichako.
Mbunge wa jimbo la Kasulu Mjini Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na wananchi wakati wa Mwenge wa uhuru ulipotembelea Mradi wa Maji wa Miji 28. Picha na Sharifat Shinji.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza wakati Mwenge wa Uhuru ulipotembelea mradi wa maji wa miji 28 katika Kata ya Msambala Halamashauri ya Mji Kasulu. Picha na Sharifat Shinji.