Buha FM Radio

Angilikana Kasulu yazindua mradi wa magari ya abiria

12 May 2026, 9:41 am

Baadhi ya magari yaliyozinduliwa na Kanisa la Angilikana Dayosisi ya Western Tanganyika wilayani Kasulu. Picha na Emily Adam.

Waumini wa Kanisa la Angilikana Dayosisi ya Western Tanganyika wilayani Kasulu waombwa kuendelea kujitolea katika uchangiiaji wa maendeleo ya kanisa hilo.

Na; Emily Adam

Kanisa la Angilikana Dayosisi ya Western Tanganyika wilayani Kasulu mkoani Kigoma limefanya uzinduzi wa mradi wa mabasi madogo ya usafiri aina ya tata unaolenga kutoa huduma ya usafirilishaji pamoja na ajira kwa kwa wakazi wa Kasuluna maeneo jirani,hali ambayo imetajwa kupunguza hali ya ukosefu wa ajira kwa vijana.

Akizungumza Asikofu wa Dayosisi ya Western Tanganyika Mhasham Emanuel Bwatta amebainisha hayo wakati akiongea kwenye hafla ya uzinduzi wa mabasi hayo uliofanyika katika viwanja vya Dayosisi hiyo Mjini Kasulu, huku hafla hiyo  ikihudhuliwa na viongozi mbalimbali wa serikali na dini,waandishi wa habari na wananchi wa kawaida.

Sauti ya MhashamEmanuel Bwatta.

Aidha askofu Bwatta ameongeza kuwa mabasi hayo matatu  aina ya tata na costa mbili yamenunuliwa kutokana na sadaka na michango ya waumini  wa kanisa la angilikana jambo ambayo amewashukuru na kuwapongeza huku akiwaasa kuendelea na moyo wa majitoleo.

Sauti ya MhashamEmanuel Bwatta.
Asikofu wa Dayosisi ya Western Tanganyika Mhasham Emanuel Bwatta akiwa na Katibu Tawala Wilaya ya Kasulu Bi.Telezia Mtewele wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi huo. Picha na Emily Adam.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Kasulu Bi.Telesia Mtewele aliyemuwakilisha mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanal Issack Mwakisu amepongeza uamuzi wa dayosisi hiyo na kutoa wito kwa taasisi za kidini wilayani humo kuendelea kushirikiana na serikali katika kubuni na kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo.

Sauti ya Katibu Tawala Bi.Telesia Mtewele.

Kanisa la Angikana Dayosisi ya Western Tanganyika wilayani Kasulu mkoani imetimiza jumla ya mabasi madogo matano ambapo yanalenga kuanzisha kampuni ya usafirishaji ya Dayosisi hiyo unatarajiwa kufanya safari zake kutoka Kasulu kwenda Tabora, Kasulu kwenda Mwanza , na Kasulu kuelekea Kigoma Mjini.

Asikofu wa Dayosisi ya Western Tanganyika Mhasham Emanuel Bwatta akizungumza mbele ya waumini wa Kanisa hilo na wananchi waliojitokeza kushuhudia uzinduzi huo. Picha na Emily Adam.