Buha FM Radio

Maafisa usafirishaji walia na bei ya Mafuta Kasulu

6 May 2026, 8:38 pm

Waendesha pikipiki kutoka Halmashauri ya Mji Kasulu. Picha na Sharifat Shinji.

Baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) kutangaza bei mpya za mafuta wafanya biashara ya Usafirishaji waeleza ongezeko hilo la bei.

Na; Helbeth Barayata

Maafisa usafirishaji alimarufu Bodaboda katika Halimashauri ya Mji Kasulu Mkoani Kigoma wamelalamikia changamoto ya kupanda kwa mafuta inayo hatarisha kipato chao.

Wakizungumuza na Buha fm radio leo kwa nyakati tofauti wamesema katika kipindi hiki wamekuwa na wakati mgumu juu ya upangaji wa bei maalumu kutokana na mfumko wa bei ya mafuta.

Sauti ya waendesha Vyombo vya Moto Kasulu.

Aidha Bodaboda hao wameiomba serikali kuweka bei rafiki na ufatiliaji wa kina kuhusu bei hizo ili kuwawezesha watumiaji wa usafiri kumudu gharama na kurahisisha biashara kwa boda boda hao.

Sauti ya waendesha Vyombo vya Moto Kasulu.

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) leo imetangaza bei mpya ya mafuta ambapo sasa lita moja ya petroli imepanda kwa Sh295 kutoka Sh 4026 hadi Sh4, 321 huku ikipanda kutoka Sh4,012 hadi Sh4,455 na mafuta ya Taa yakipanda kutoka Sh3,891 hadi Sh4,884 kwa Wilayani Kasulu.