Sirro aipongeza Kasulu kwa Hati safi ya CAG
Buha FM Radio

Sirro aipongeza Kasulu kwa Hati safi ya CAG

23 July 2026, 10:45 am

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi SAimon Sirro wakati akizungumza na Madiwani wa Halmashauri ya Mji Kasulu. Picha na Irene Charles.

Mkuu wa Mkoa wa Kigma Balozi Saimon Sirro ameitaka Halmashauri ya Mji Kasulu kuendelea kuimarisha usimamizi wa fedha za umma, kuyafanyia kazi mapendekezo ya CAG kwa wakati na kudumisha uwajibikaji kwa wananchi.

Na; Irene Charles

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Balozi Simon Sirro, ameipongeza Halmashauri ya Mji Kasulu kwa kupata hati safi katika Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2025/2026, pamoja na kufikia asilimia 98 ya ukusanyaji wa mapato ya ndani.

Akizungumza katika Mkutano Maalum wa Baraza la Madiwani uliojadili ripoti na mapendekezo ya CAG, Balozi Sirro amesema mafanikio hayo yanaonyesha uwajibikaji na usimamizi mzuri wa rasilimali za umma unaofanywa na viongozi pamoja na watumishi wa Halmashauri hiyo.

Sauti ya Balozi Sirro.
Baadhi ya Madiwani wa Halamshauri ya Mji Kasulu na Wadau mbalimbali wa Maendeleo wakiwa katika mkutano wa Halimashauri hiyo. Picha na Irene Charles.

Aidha, Balozi Sirro amesisitiza umuhimu wa kuimarisha ulinzi na usalama, akiwataka madiwani na viongozi wengine kuhakikisha sheria za nchi zinafuatwa, hususan katika udhibiti wa watu wanaoingia na kutoka nchini. Ameagiza watendaji kushirikiana kwa karibu na Idara ya Uhamiaji pamoja na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ili kuendelea kulinda amani na usalama wa wananchi.

Sauti ya Balozi Sirro.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kasulu, Ayubu Ngaraba, amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa ushauri na maelekezo aliyoyatoa. Amesema Halmashauri itayafanyia kazi mapendekezo yote yaliyomo kwenye ripoti ya CAG ili kuondoa dosari zilizobainishwa na kuendelea kuboresha usimamizi wa fedha na utoaji wa huduma kwa wananchi.

Sauti ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kasulu, Ayubu Ngaraba.
Baadhi ya Madiwani wa Halamshauri ya Mji Kasulu na Wadau mbalimbali wa Maendeleo wakiwa katika mkutano wa Halimashauri hiyo. Picha na Irene Charles.