Buha FM Radio

Ushirikiano wa wanandoa katika upangaji wa bajeti za familia

6 June 2026, 6:51 pm

Familia ikipanga bajeti ya familia. Picha kwa muujibu wa Akili Unde Chatgpt

Kutokana na takwimu na machapisho mbalimbali kuhusu umhimu wa kupanga bajeti kwa wanandoa na familia kwa ujumla Buha FM Radio imeangazia umhimu wa wanandoa kushirikiana katika upangaji wa bajeti.

Imeandaliwa na Timu nzima ya Makala ya kipindi chetu leo

Kwa muujibu wa Utafiti wa 5, mwaka 2023 wa FinScope Tanzania ulioratibiwa na Financial Sector Deepening Trust Tanzania kwa kushirikiana na Bank kuu ya Tanzania na shirika la Takwimu Tanzania umeonyesha kuwa usimamizi wa fedha za familia na upangaji wa matumizi ni sehemu muhimu ya ustawi wa kaya na maendeleo ya uchumi wa taifa.

Hata hivyo chapisho la Serikali kupitia Bank kuu ya Tanzania na Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali wa mwaka 2024/2025, asilimia ya Watanzania wanaotumia huduma rasmi za kifedha iliongezeka kutoka asilimia 65 mwaka 2017 hadi asilimia 76 mwaka 2023, hali iliyochangiwa na kuongezeka kwa elimu ya fedha, matumizi ya teknolojia ya kifedha na usimamizi bora wa matumizi ya kaya, licha ya hivyo baadhi Mkala ya Kipindi chetu leo imelitaza jambo hili kwa upana kutaka kufahamu endapo familia zinapanga bajeti kwa kushiriiana.