Buha FM Radio

Jamii yaonywa unyanyapaa na ukatili kwa watoto

April 23, 2025, 4:03 pm

Mwanafunzi mwenye ulemavu akieleza changamoto anazopitia. Picha na Shinji

Wanafunzi wenye changamoto ya ulemavu wamesimulia wanavyopitia changamoto mbalimbali wanapokuwa shuleni.

Na Sharifat Shinji

Wananchi katika Halmashauri ya Mji Kasulu mkoani Kigoma wameombwa kutojihusisha na vitendo vya Unyanyapaa kwa Watu wenye Ulemavu pamoja na kutojihusisha katika vitendo vya  ukatili kwa watoto waliopo shuleni  ili Kujenga  usitawi na maendeleo bora katika jamii.

Hayo yamesemwa leo na  Kamishna wa Elimu Tanzania Dkt. Lyabwene Mtahabwa wakati akizungumza katika Hafula ya  Kongamano la uzinduzi wa program ya utafiti tatuzi kuhusu Usalama Jumuishi katika Elimu lililofanyika katika Kiwanja cha Mpira Kiganamo na kusisitiza jamii inawalinda watoto wote wenye ulemavu na wasio na ulemavu ili kujenga jamii bora.

Sauti ya Dkt. Lyabwene Mtahabwa

Aidha Dkt. Mtahabwa amesema watu wote wanaojihusisha na kuwanyanyasa  na kusababisha kukosekana kwa usalama, ustawi  na maendeleo ya motto atachukuliwa hatua kali za kisharia ili kuhakikisha anakuwa mfano kwa watu waote watakaokiuka taratibu hizo.

Awali Kaimu Katibu Tawala mkoa wa kigoma Bi. Paulina Ndigeza ameshukuru na kumpongeza Dkt.  Lyabwene Mtahabwa  kuwa mgeni rasimi katika Hafla hiyo na kusema Mkoa wa kigoma inao watoto wanaosoma katika shule jumuishi huku akiahidi mkoa wa kigoma na mikoa mingine mitatu iliyoteuliwa kufanya utafti huo kuwa wataufanyia kazi vizuri.

Sauti ya Kaimu Katibu Tawala mkoa wa kigoma Bi. Paulina Ndigeza

Katika hatua nyingine Ndize Juma ambaye ni mwanafunzi mwenye ulemavu kutoka shule ya Sekondari Kigoma Grand amesema wananchi na jamii kwa ujumla  wanapaswa kuacha tabia ya kuwanyanyapaa watu wenye ulemavu hasa katika swala la elimu.

Mpango wa Programu ya Utafiti Tatuzi Kuhusu Usalama Jumuishi katika Elimu umezinduliwa leo chini ya taasisi ya Elimu Bora nchini ikiwa na lengo la kuwasaidiwa watoto wote nchini wenye ulemavu na wasio na ulemavu wanapata elimu bora bila changamoto yoyote ya unyanyapaa pamoja na ukatili juu yao.