Buha FM Radio

Magonjwa yasiyo ya kuambukizwa yatajwa kuwa janga la Dunia

21 April 2026, 10:44 pm

Dkt. Simon Mtekwa Mratibu wa magojwa yasiyo ya kuambukizwa na magojwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele katika Halmashauri ya Mji Kasulu. Picha Helbeth Barayata.

Daktari Simon Mtekwa amesema magonjwa yasiyoyakuambukiza yameendelea kuisumbua dunia kwa sasa.

Na; Helbeth Barayata

Wananchi wa Halmashauri ya Mji Kasulu Mkoani Kigoma waaswa kujikinga na magojwa yasiyo ya kuambukizwa kwa kuchukua tahadhari ya lishe, mazoezi na uchunguzi wa afya mara kwa mara ili kulinda afya zao.

Akizungumza na Buha FM Radio leo kupitia kipindi cha Darasa nje ya shule Dkt. Simon Mtekwa Mratibu wa magojwa yasiyo ya kuambukizwa na magojwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele katika Halmashauri hiyo amesema magojwa hayo yamekuwa yakichangia  kwa asilimia 71 kwa vifo vyote duniani.

Sauti ya Dkt. Simon Mtekwa.

Hata hivyo ameeleza zaidi katika ugojwa wa kisukari na kusema ugojwa huo hutokea pale kongosho inaposhambuliwa na kushidwa  kuratibu kiwango cha sukari mwilini hali inayopelekea mhanga kupata ugojwa huo huku akibainisha dalili za ugonjwa huo na kuwasihi wananchi kuchukua tahadhari ya kufanya vipimo.

Sauti ya Dkt. Simon Mtekwa.

Kwa upande wake afisa lishe kutoka Halmashauri hiyo Ndug. Mwita Range amesema katika kujikinga na ugojwa wa kisukari wananchi wanapaswa kuzingatia lishe bora na kupunguza milo ya mara kwa mara pamoja na mambo mbalimbali wanayopaswa kuyafuata ili kujiepusha na magonjwa hayo.

Sauti ya Mwita.

Katika kupambana na magojwa yasiyo ya kuambukizwa dakitari ametoa wito kwa jamii kuzingatia muda wa kupumzika, huku akibainisha muda wa watoto wa miaka 6 -13  kulala masaa 9 -11, wenye umri wa miaka 14-17 walale masaa 8-10, watu wazima miaka 18 -64 walale masaa 7 -9 na wazee miaka kati ya 65- na kuendelea walale masaa 7 -8  na kusema ili kupata usingizi mzuri ni mhimu kupumzika eneo lenye utulivu na hewa safi.