Buha FM Radio

Redcross Kaulu yafanya uchaguzi wa viongozi

21 June 2026, 2:14 pm

Baadhi ya wananchama na Viongozi wa Chama Cha Msalaba Mwekundu wilayani Kasulu. Picha na Emily Adam.

Wananchi wilayani Kasulu wahimizwa kujiunga katika Chama Cha Msalaba Mwekundu kikitajwa kuwa kina mchango mkubwa katika jamii.

Na; Emily Adam

Chama cha Msalaba Mwekundu Redcross Tawi la Mjini  na Mrusi,  Halmashauri ya Mji Kasulu Mkoani Kigoma kimefanya uchaguzi wa viongozi  katika nafasi mabimbali wakiwemo Mwenyekiti, Mwakilishi wa vijana pamoja na wanawake na kuahidi kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa baina yao na wanachama ili kufanikisha malengo ya chama hicho.

Uchaguzi huo umefanyika shule ya msingi Kasulu ambapo baada ya Wilibroad John Mlazi kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa tawi la Kasulu Mjini  amewashukuru wanachama kwa kumchagua kwa kura zote kuahidi kuwa atafanya kazi kwa waledi kama katiba yao inavyoelekeza.

Sauti ya Mwenyekiti Tawi la Mjini Wilibroad Mlazi.

Aidha amesema Redcross ina lengo la kuhudumia jamii kwa kushirikiana na serikali katika majanga mbalimbali kama vile mlipuko ya magonjwa pamoja  na mambo mengine.

Sauti ya Mwenyekiti Tawi la Mjini Wilibroad Mlazi.

Kwa upande wake mwenyekiti wa tawi la mrusi Anjero Prosper Tungalaza  ametoa wito kwa wananchi kutambua mchango wa Redcross katika maeneo yao na kujiunga na chama hicho kwani kina umuhimu mkubwa katika jamii.

Sauti ya Mwenyekiti wa Tawi la Mrusi Anjero Prosper.

Katika hatua nyingine Mwakilishi wa wanawake Justina Elisha Chija na mwakilishi wa vijana  Issack Ntacho wamesema chama cha msalaba mwekundu Redcross kimekuwa mkombozi kwa wanawake hasa wajawazito wanaojifungua na kupoteza damu nyingi pamoja na wahanga wa ajali kwa kujitolewa damu kwa asilimia kubwa.

Sauti za wawakilishi Wanawake na Vijana.

Jumla ya wanachama 24 wa Msalaba Mwekundu Tawi la Kasulu Mjini na 20 kutoka Mrusi wameshiriki katika kuchagua viongozi hao ambao wataendelea kutoa ushirikiano ili kuimarisha na kudumisha chama hicho chenye mchango mkubwa ndani ya jamii na taifa kwa ujumla.