Buha FM Radio

Kasulu Mji yatoa Milioni 265 kwa vikundi 24

2 July 2026, 1:13 pm

Baadhi ya wanufaika wa mikopo ya Asilimia 10 ya Halmashauri ya Mji Kasulu wakiwa katika ukumbi wa Halmashauri hiyo. Picha na Emily Adam.

Prof. Ndalichako Mbunge wa Jimbo la Kasulu Mjini awasisitiza wanufaika wa mikopo ya Asilimia 10 kurejesha kwa wakati mikopohiyo ili iwanufaishe na waengine.

Na; Emily Adam

Zaidi ya Milioni 261 zimatolewa kwa kwa vikundi 24 vya wanawake, vijana na Walemavu ambavyo vinajishughukisha na kazi mbalimbali katika Halmashauri ya Mji Kasulu mkoani Kigoma ikiwa ni mikopo ya asilimia kumi ya mapato ya ndani ili kusaidia kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza Mgeni rasmi katika hafla ya utoaji wa mikopo hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashari hiyo  Mbunge wa jimbo la Kasulu Mjini Prof. Joyce Ndalichako amesema mikopo hiyo imetolewa kwa vikundi vilivyokidhi vigezo na kuwaasa wanufaika kuirejesha kwa wakati bila usumbufu ili kutoa fursa ya kuendelea kukopesha vikundi vingine.

Sauti ya Prof. Ndalichako 1

Aidha Prof. Ndalichako amesema asilimia kubwa ya fedha zilizotelewa katika mikopo hiyo ni marejesho ya mikopo ya awali huku akieleza hali ya urejeshaji wa mikopo hiyo katika Halmashauri ya Mji Kasulu kuwa imeimalika na kusisitiza vikundi vilivyochukua mikopo hiyo kurejesha kwa wakati bila usumbufu.

Sauti ya Prof. Ndalichako 2
Mgeni rasmi katika hafla ya utoaji wa mikopo hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashari ya Mji Kasulu  Mbunge wa jimbo la Kasulu Mjini Prof. Joyce Ndalichako. Picha na Emily Adam.

Awali akitoa taarifa fupi ya utoaji wa mikopo, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu ambaye pia ni mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii  Azizi Ndalfa Sindeye  amesema kiasi kilichotolewa kilitengwa katika kipindi cha robo ya nne ya mwaka wa fedha wa 2025/2026.

Sauti ya Sindeye.

Kwa upande wao wanufaika wa mikopo hiyo wameishukuru serikali kwa kuendelea kuunga mkono jitihada zao huku wakisema mikopo hiyo itawanufaisha kiuchumi kupitia shughuli wanazozifanya huku wakiahidi kutumia fedha hizo kwa malengo waliyoyakusudia na kurejesha kwa wakati.

Sauti za wanufaika wa mikopo ya Asilimia 10.
Miongoni mwa waemavu na wanufaika wa mikopo ya asilimia 10 ya mikopo ya Halmashauri ya Mji Kasulu. Picha na Emily Adam.

Halmashauri ya Mji Kasulu imekuwa ikitoa 10% ya mapato yake ya ndani kwa vikundi hivyo lengo ikiwa ni kuinua na kukuza kipato kwa wananchi wake na Taifa kwa ujumla.