Buha FM Radio
Buha FM Radio
6 June 2026, 5:05 pm

Shirika la TAWEN limesema limejipanga kuwawezesha wananwake wa Halmashauri ya Mji Kasulu kiuchumi na kuachana na vikundi vya vikomba ambavyo vimekuwa changamoto kwa baadhi familia.
Na; Irene Cherles
Katibu Tawala Halmashauri Mji Kasulu Bi.Theresia Mtewele amesema elimu ya ujasiriamali ndio ufunguo wa kukabiliana na umasikini akitaja kuwa Selikari imefungua milango mingi ya kiuchumi kwa wananchi wake.
Akizungumza katika halfla ya uzinduzi wa TAWEN (Tanzania Women Empowerment Network) mkoa wa kigoma ulioambatana na semina ya nishati safi ya kupikia pamoja na elimu ya ujasiliamali Theresia amesema Mafunzo hayo yamekuja kufungua njia na kuvutia wadau wengi kwaajili ya kuleta maarifa kutokana na rasilimali zilizopo.
Aidha amevisistiza vikundi vya wanawake na vijana kutofanya biashara kwa mazoea bali waunde vikundi rasmi na kujisaji katika Halmashauri au ofisi za kibenki kwa lengo la kupata mitaji.

Kwa upande wake mwenyekiti wa wa TAWEN Bi. Silesi Mali amesema maono TAWEN ni kuwawezesha wanawake na vijana kiuchumi kwa kuwaonesha fursa zilipo ndani ya Wilaya ya Kasulu pamoja na kuwapatia elimu ya kuendeleza miradi inayotokana na fursa hizo.
Katika hatua nyingine Mali amesema changamoto kubwa iliyopo kwa sasa wanawake wengi wameegemea kwenye vikoba ambavyo vimesababisha migogoro katika familia huku akiwasisitiza wananchi watakaofika TAWEN wawe na wazo la biashara ya kufanya.

Kwa upande wao baadhi ya washiriki wamesema kupitia semina hiyo wamejifunza vitu vingi huku wakiomba Selikari kuendelea kutoa elimu juu ya upataji wa mikopo pamoja na matumizi sahihi ya nishati safi.
TAWEN ina jukumu la kutoa taarifa za kibiashara, maonesho, uandaji wa makongamano lengo ni kuwajengea uwezo Wanawake kupitia mafunzo mbalimbali pamoja na kuwapatia masoko yenye uhakika.