Buha FM Radio
Buha FM Radio
20 July 2026, 5:23 pm

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Kasulu, Dkt. Nangi William amewasisitiza wananchu kutumi lishe bora na mlo kamili pamoja na kujiepusha na matumizi ya pombe na sigara ili kulinnda afya zao.
Na; Emily Adam
Wananchi wa Halmashauri ya Mji Kasulu mkoani Kigoma wamehimizwa kuzingatia ulaji wa lishe bora kwa kutumia mlo kamili, pamoja na kujiepusha na matumizi ya pombe kupita kiasi, uvutaji wa tumbaku, ili kulinda afya zao na kujiepusha na magonjwa yasiyoambukiza.
Wito huo umetolewa na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Kasulu, Dkt. Nangi William, alipomwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Issack Mwakisu, katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya uchangiaji wa damu salama iliyofanyika Hospitali ya Mji Kasulu Mlimani iliyoandaliwa na Jumuiya ya JAI.
Akizungumza katika hafla hiyo, Dkt. William amesema wananchi wengi bado hawazingatii matumizi sahihi ya vyakula vyenye lishe bora, huku baadhi yao wakiendelea kutumia pombe na tumbaku kupita kiasi, hali inayochangia kuongezeka kwa matatizo mbalimbali ya kiafya.
Aidha Dk. Wiliam amewasa wakazi wa MJi wa Kasulu kujiepusha na vyakula vyenye mafuta mengi kupita kiasa pamoja na kuzingatia kanuni bora za afya sambamba na kufanya mazoezi ya mara kwa mara ili kjilinda na kujikinga na magongwa yasiyo ambukizwa.

Katika hatua nyingine Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Mji Kasulu Mlimani Dkt. Telesphol Paschal amesema katika zoezi hilo jumla ya unit 150 za damu salama zimepaikana ambazo zitatumika kuokoa maisha ya watu wenye mahitaji ya damu kama vile wahanga wa ajari na akinamama wanaojifungua na kupoteza damu nyingi katika hosipitali hiyo.