Buha FM Radio
Buha FM Radio
9 June 2026, 11:52 am
Sekretarieti ya maadili imeeleza jinzi inavyofanya kazi kwa muujibu wa sheria za jamhuri ya muungano wa Tanzania huku ikieleza majumumu iliyonayo katika usimamizi wa maadili ya viongozi wa Umma.
Na: Sharifat Shinji
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma imeanzishwa kwa mujibu wa Ibara ya 132 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Sura 398 ikiwa ni Idara ya serikali inayojitegemea chini ya Ofisi ya Rais.
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ni chombo kinachosimamia maadili ya viongozi wa umma, kwa mujibu wa Ibara ya 132 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma imepewa jukumu la kuchunguza Tabia na Mienendo ya kiongozi yeyote wa umma, kwa madhumuni ya kuhakikisha kwamba masharti ya sheria ya maadili ya viongozi wa umma, yanazingatiwa na viongozi husika kama anavyoeleza hapa Afisa maadili kanada ya Magharibi Tabaora. Bwana Vupala Mbwilo.