Kasulu washauriwa migogoro ya ardhi isuluhishwe na mamlaka husika
Buha FM Radio

Kasulu washauriwa kutumi mamlaka kusuluhisha migogoro ya ardhi

4 June 2026, 11:48 am

Mratibu wa polisi jamii Wilaya ya Kasulu na mkaguzi msaidizi wa polisi na polisi jamii kata ya Nyamunyusi Asp/Insp. Willy Lupa akizungumza katika kipidi cha Darasa Nje ya Shule.

Mratibu wa polisi jamii Wilaya ya Kasulu na mkaguzi msaidizi wa polisi na polisi jamii kata ya Nyamunyusi Asp/Insp. Willy Lupa amewasisitiza wananchi wanaokumbana na migogoro ya aridhi kusuluhisha katika mamalaka husika kabla ya kufikishana polisi.

Na; Paulina Majaliwa

Wananchi wilayani Kasulu mkoani Kigoma wameshauriwa kusuluhisha migogoro ya ardhi katika mamlaka zinazohusiana na maswala ya ardhi zinazopatikana katika maeneo yao.

Hayo yamesemwa na mratibu wa polisi jamii Wilaya ya Kasulu na mkaguzi msaidizi wa polisi na polisi jamii kata ya Nyamunyusi Asp/Insp. Willy Lupa wakati akizungumza na Buha fm radio ambapo amesema kuwa kabla hawajafika katika jeshi la polisi watumie mabaraza ya usuluhishi ya ardhi ngazi ya kata,baraza la nyumba na ardhi la wilaya pamoja na mahakama kuu divisheni ya ardhi ili kupata usuluhishi zaidi.

Sauti ya Insp. Willy Lupa 1.

Aidha amesema kabla hawajafika kituo cha polisi ni lazima wapite kwenye mamlaka zinazohusiana na mausala ya ardhi ili kupata urahisi wa kusuluhisha migogoro hiyo katika njia ya Amani na utulivu kwa wahusika wa migogoro hiyo.

Sauti ya Insp. Willy Lupa 2.

Katika hatua nyingine amesema ni lazima kwa kila mtu anayepeleka shauri la madai ya migogoro ya ardhi anatakiwa kutunza nyaraka za shauri hilo ili kuipa urahisi mamlaka hiyo endapo itatokea mmoja wa wahusika wa kesi hiyo hajaridhika na maamuzi ya hapo awali.

Sauti ya Insp. Willy Lupa 3.

Lupa ameitaka jamii kuepuka kusuluhisha migogoro ya ardhi ndani ya jamii pasipo kufuata taratibu zinazotakiwa kwani baadhi yao wamekuwa kisuluhisha migogoro hiyo kwa makubaliano yao wenyewe bila kuhusisha viongozi jambo linalopelekea madhara mengine katika jamii.

“Niwashauri wananchi wajiepushe na maswala ya kusuluhisha migogoro ya ardhi kwa njia za kienyeji za kumaliza migogoro hii wao kwa wao bila kushirikisha viongozi kwani jambo hili linaweza kupelekea kuzalishwa kwa migogoro mingine” Amesema Lupa.

Mratibu wa polisi jamii Wilaya ya Kasulu na mkaguzi msaidizi wa polisi na polisi jamii kata ya Nyamunyusi Asp/Insp. Willy Lupa akizungumza katika kipidi cha Darasa Nje ya Shule.

Migogoro ya ardhi ni miongoni mwa matatizo yanayojitokeza mara kwa mara kutokana na umiliki, matumizi, na mipaka ya ardhi huku sababu kuu za migogoro hiyo ikitajwa kuwa  ukosefu wa hati miliki, uvamizi wa ardhi, na kutokuelewana kati ya familia au majirani hivyo kupitia msaada wa kisheria, wananchi wanapewa elimu kuhusu.