Buha FM Radio

Migogoro ya ndoa inavyozima ndoto za wanafunzi shuleni

5 October 2026, 12:09 pm

Baadhi ya wanafuzi wa kike wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Wasichana Mavuno wakiwa katika Mahafali ya 12 ya shule hiyo. Picha na Sharifat Shinji.

Kutokana na Serikali kutambua umhimu wa elimu kwa watoto, baadhi ya wadau wa elimu wamekuwa wakitaja kuwa migogoro ya ndoa na familia imekuwa ikichangia kushuka kwa ufaulu wa wanafunzi na baadhi kushindwa kuendelea na masomo kabisa.

Na; Sharifat Shinji

Mkurugenzi wa shule ya sekondari ya Wasichana Mavuno Ndg. Gaston Samweli amewahimiza wazazi na walezi kutowahusisha watoto katika changamoto za ndoa na familia wakati wa masomo jambo litakalowasaidia kufanya vizuri katika mitihani ya kitaifa inayaotarajiwa kufanyika mwezi huu.

Ameyasema hayo wakati wa Maafali ya 12 ya shule ya Sekondari ya Wasichana Maavuno wilayani Kasulu mkoa wa Kigoma ambapo amesema kuna baadhi ya wazazi na walezi wamekuwa na tabia ya kuwahusisha watoto wa shule na migogoro ya familia jambo linalopelekea wanafunzi kushindwa kufanya vizuri darasani.

Sauti ya mkurugenzi Gaston.

Aidha Gaston amewasisitiza wazazi na wanafunzi kusimamia swala la nidhamu katika familia akiwaonya kujihusisha na mambo ya ulevi na starehe chini ya umri pamoja na kuwaonya wazazi kuwahusisha watoto katika mambo yasiyofaa.

Sauti ya mkurugenzi Gaston.
Mkurugenzi wa shule ya Sekondari ya Wasichana Mavuno Ndg. Gaston Mavuno. Picha na Sharifat Shinji.

Kwa upande wake Mgeni rasimi wa Mahafali hayo Mthibiti Mkuu Ubora wa shule Mstafu Lay Canon amewaasa wazazi kuviendeleza vipaji vya watoto kwa kuwapeleka katika vyuo vya ufundi wakiwa wanasubili kuendelea na elimu ya kidato cha tano na vyuo vya kati.

Sauti ya Lay Canon.
Mgeni rasimi wa Mahafali 12 katika shule ya Sekondari ya Wasichana Mavuno Mthibiti Mkuu Ubora wa shule Mstafu Lay Canon. Picha na Sharifat Shinji.

Nao baadhi ya wazazi  akiwemo Adriano Ntibagomba  na Hekima Kalimanzila wamekili uwepo wa poromoko la maadili katika jamii huku wakishauri wazazi kuwajibika huku wakisistiza watoto kupewa elimu ya ufundi ili kuepuka mrundikano wa vijana wasio na kazi maalumu.

Sauti za wazazi.
Baadhi ya wazazi na walezi katika mahafali ya 12 ya shule ya Sekondari Wasichana Mavuno. Picha na Sharifat Shinji.