Buha FM Radio

Utoaji wa taarifa za ukatili bado changamoto Kasulu

12 October 2026, 1:29 pm

Mkuu wa dawati la jinsia na ulinzi wa watoto Wilayani Kasulu Inspector Maimuna Omar. Picha na Sharifat Shinji.

Mkuu wa dawati la jinsia na ulinzi wa watoto Wilayani Kasulu Inspector Maimuna Omar ameeleza kuwa utoaji wa taarifa za matukio ya ukatili wa kijinsi katika jamii bado ni changamoto kutokana na wananchi kuhofia usalama wao baada ya kutoa taarifa hizo.

Na; Ramadhan Zaidy

Wananchi wilayani Kasulu mkoani Kigoma wametakiwa kujenga tabia ya kuripoti matukio na vitendo vya ukatili wa kijinsia wanaofanyiwa katika jamii ili kupatiwa msaada na kupunguza matukio hayo katika jamii.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa dawati la jinsia na ulinzi wa watoto Wilayani Kasulu Inspector Maimuna Omar wakati akizungumza na Buha FM Radio, na kusema kuripoti matukio hayo kunasaidi mhanga kupatiwa msaada mapema kabla ya kuathirika zaidi.

Sauti ya Inspector Maimuna.

Aidha Inspector Maimuna amewataka wazazi na walezi kuwa walinzi wa kwanza, kuendelea kutoa elimu kwa watoto wao ili kukabiliana na matukio ya ukatili katika familia.

Sauti ya Inspector Maimuna.

Katika hatua nyingine Inspestor Maimuna ametoa maelekezo naana ya kuripoti na kutoa taarifa ya matukio hayo akisema, kituo cha polisi ni sehemu moja wapo ya kutoa taarifa hizo pamoja na Ofisi ya Mtendaji wa mtaa, Viongozi wa serikali za mitaa na vijiji.

Sauti ya Inspector Maimuna.
Mkuu wa dawati la jinsia na ulinzi wa watoto Wilayani Kasulu Inspector Maimuna Omar. Picha na Sharifat Shinji.

Disemba 10, 2024 katika kilele cha maadhimisho ya siku 16 ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto yaliyofanyika Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma afisa usitawi wa jamii Mkoa wa Kigoma Bw. Petro Bwanji alisema zaidi ya matukio 1900 ya ukatili wa wanawake na watoto kwa mwaka 2022/2023 mkoani Kigoma yalilipotiwa.