Buha FM Radio

Abiria watakiwa kuandikisha majina halisi kwenye tiketi za usafiri

22 November 2026, 10:32 am

Mkuu wa kitengo cha usalama barabarani wilayani Kasulu mkoani Kigoma SP Patrick Damas akitoa elimu ya usalama barabani. Picha na Emily Adam.

Abiria wana wajibu mkubwa wa kulinda usalama wao wapokuwa safarini  pamoja na kudhibiti uvunjaji wa sheria za usalama barabarani kwa kushirikiana na jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa jeshi hilo.

Na; Emily Adam.

Mkuu wa kitengo cha usalama barabarani wilayani Kasulu mkoani Kigoma SP Patrick Damas ametoa wito kwa abiria wanaosafiri kwa mabasi wilayani humo kuhakikisha wanaandikisha majina yao halisi kwenye tikeki zao pamoja na kuzingatia taratibu zote za usafiri.

SP Damas ametoa rai hiyo wakati akizungumza na Buha FM Radio kupitia kipindi cha shangwe la asubuhi na ameeleza kuwa abiria wanatakiwa kukata tiketi mapema na kuhakikisha ina jina kamili ya msafiri, namba ya gari, mawasiliano ya mmiliki wa basi pamoja na kuzingatia muda sahihi wa kuanza safari.

Sauti ya Mkuu wa kitengo cha usalama barabarani wilayani Kasulu mkoani Kigoma SP Patrick Damas

Aidha SP Damas ameongeza kuwa kuna baadhi ya abiria wanaoshindwa kutoa taarifa sahihi ikiwemo kuandikisha majina yasiyo halisi na mizigo walionayo jambo ambalo linaweza kuleta usumbufu mkubwa na kusababisha abiria aliyedanganya taarifa zake kukosa haki yake wakati wa kulipwa fidia inapotokea dharula kama vile ajali na upotevu wa mizigo.

Sauti ya Mkuu wa kitengo cha usalama barabarani wilayani Kasulu mkoani Kigoma SP Patrick Damas

Abiria wana wajibu mkubwa wa kulinda usalama wao wapokuwa safarini  pamoja na kudhibiti uvunjaji wa sheria za usalama barabarani kwa kushirikiana na jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani kwa kutao taarifa kwa jeshi hilo ili kutokomeza ajali za barabarani zinazosababishwa na uzembe wa baadhi ya watu.