Buha FM Radio

Wananchi watakiwa kuchagua vyakula bora kwa kujenga afya

21 November 2026, 3:45 pm

Afisa lishe kutoka Halmashauri ya wilaya ya Kasulu Bi. Subira Swai akieleza umuhimu wa lishe bora katika kuimarisha afya ya mwili. Picha na Emily Adam.

Matumizi ya bidhaa za chakula zilizoisha muda wake na ambazo hazina virutubisho vya kutosha yanaweza kupelekea mlaji kukosa madini na vitameni muhimu vinavyopatikana kwenye chakula husika na wakati mwingine kumsababishia madhara mbalimbali ya kiafya.

Na; Emily Adam.

Jamii wilayani Kasulu mkoani Kigoma imeshauriwa kutumia vyakula vilivyoongezewa virutubisho na vile vya asili pamoja na kula mlo kamili katika utaratibu wa ulaji wa vyakula wa kila siku ili kujenga mwili na kuongeza madini muhimu mwilini.

Wito huo umetolewa na Afisa lishe kutoka Halmashauri ya wilaya ya Kasulu Bi. Subira Swai wakati akizungumza na Buha FM Radio na kusema vyakula vilivyorutubishwa havichukui nafasi za vyakula vingine kwenye mlo wa familia bali ni jitihada zinazofanywa ili kuhakikisha jamii inapata na kutumia chakula bora zaidi.

Sauti ya Afisa lishe kutoka Halmashauri ya wilaya ya Kasulu Bi. Subira Swai

Ameeleza kuwa uratubishaji wa chakula unaofanywa na mamlaka husika unalenga kuongeza madini na vitameni mbalimbali kama vile madini chuma, phoric Acid na zinc pamoja na vitameni ambavyo ni muhimu katika mwili wa binadamu.

Sauti ya Afisa lishe kutoka Halmashauri ya wilaya ya Kasulu Bi. Subira Swai
Afisa lishe kutoka Halmashauri ya wilaya ya Kasulu Bi. Subira Swai akizungumza na Buha FM Radio. Picha na Emily Adam.

Katika hatua nyingine Bi Swai amewaasa wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Kasulu kuwa na desturi ya kusoma na kupata maeelezo ya kina katika bidhaa za vyakula hususani kuangalia muda wa matumizi ya bidhaa husika ili kuepuka kutumia bidhaa zisizo na ubora na zilizo isha muda wake.

Sauti ya Afisa lishe kutoka Halmashauri ya wilaya ya Kasulu Bi. Subira Swai.

Matumizi ya bidhaa za chakula zilizoisha muda wake yanaweza kupelekea mlaji kukosa madini na vitamini muhimu vinavyopatikana kwenye chakula husika na wakati mwingine kumsababishia madhara mbalimbali ya kiafya.