Buha FM Radio

Huzuni yatawala makabidhiano ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Kasulu

9 October 2026, 1:10 pm

Kushoto Mkuu wa Wilaya aliyepita Mhe. Kanali Isaac Mwakisu na kulia Mkuu wa Wilaya mpya Luteni Kanali Joseph Murimi wakikabidhiana nyaraka za ofisi ya Mkuu wa Wilaya. Picha na Sharifat Shinji.

Baada ya kuitumikia kwa kipindi cha miaka mitano na miezi mitatu aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Isac Mwakisu amewaaga rasmi viongozi na wananchi akiwashukuru kwa ushirikiano waliompatika kwa kipindi chote cha utumishi wake ndani ya Wilaya hiyo.

Na; Saharifat Shinji

Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma imefanya hafla ya makabidhiano ya ofisi kati ya Mkuu wa Wilaya aliyepita Mhe. Kanali Isaac Mwakisu na Mkuu wa Wilaya mpya Luteni Kanali Joseph Murimi tukio lililohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Wiaya ya Kasulu na wananchi.

Akizungumza katika hafla hiyo Katibu Tawala wa Wilaya ya Kasulu Bi. Telesia Mtewele amesema makabidhiano hayo ni sehemu ya taratibu za kiutawala na kiutamaduni huku akimshukuru Kanali Isaac Mwakisu kwa utumishi wake ndani ya Wilaya hiyo na kumkaribisha Mkuu mpaya Luteni Kanali Joseph Murimi katika majukumu yake mapya ndani ya Wilaya ya Kasulu.

Sauti ya katibu Tawala Wilaya ya Kasulu.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kasulu Bi. Telesia Mtewele. Picha na Sharifat Shinji.

Kwa upande wake aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Kanali Isaac Mwakisu amewaaga rasmi viongozi, watumishi na wananchi wote wa Wilaya ya Kasulu akiwashukuru kwa ushirikiano waliompa katika kipindi chote cha uongozi wake na kuwaomba viongozi na wananchi kumpa ushirikiano huo huo Luteni Kanali Murimi.

Sauti ya Kanali Isaac Mwakisu.

Nae Mkuu wa Wilaya mpya ya Kasulu Luteni Kanali Joseph Murimi ameahidi kufanya kazi kwa kufuata sheria zinazomwongoza huku akiwaomba wananchi na watumishi wa serikali kusimama upande wake ili wafanye kazi kwa ushirikiano.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya mpya ya Kasulu Luteni Kanali Joseph Murimi
Mkuu wa Wilaya mpya ya Kasulu Luteni Kanali Joseph Murimi. Picha na Sharifat Shinji.

Katika hatua nyingine mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kasulu Mbelwa Chidebwe amesema kufanya kazi kwa muda mrefu na kwa ushirikiano kumeacha huzuni kwa watu wengi huku akimshauri mkuu wa wilaya mpya kutumia timu iliyopo kuiongoza Wilaya ya Kasulu.

Sauti ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kasulu Mbelwa Chidebwe.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kasulu Mbelwa Chidebwe. Picha na Sharifat Shinji.

Kwa upande wao viongozi wa vyama vya siasa wilayani Kasulu wakiwakilishwa na Haruna Kwasakwasa wa chama ICT. Wazalendo ameeleza namna walivyoshirikiana na Kanali Mwakisu huku akiahidi ushirikiano kwa Mkuu mpya Luteni Kanali Murimi.

Sauti ya Haruna Kwasakwasa.
Baadhi ya viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Kasulu wakiwa katika hafla ya makabidhiano ya ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kasulu. Picha na Sharifat Shinji.

Kanali Mwakisu amehamishwa kituo cha kazi kutoka kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma, kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Misenyi Mkoani Kagera.