Buha FM Radio
Buha FM Radio
17 November 2026, 11:57 am

Mwalimu Wenseslaus Justine Lugaya ambaye amepanga kuanza ziara ya kutembelea mikoa 21 ya Tanzania Bara na mikoa 5 visiwani kwa kutumia Baiskeli iki kuhamasisha upandani wa miti zaidi ya Milioni moja na laki tato ili kukabiliana na mabadiliko ta tabianchi na utunzaji wa mazingira kuanzia Novemba 16, 2027 hadi Februali 16, 2027.
Na; Khadija Shabani
Halmashauri ya mji Kasulu mkoani Kigoma imemuaga rasmi Mwalimu Wenseslaus Justine Lugaya ambaye ameanza ziara ya kutembelea mikoa 31 ya Tanzania Bara na visiwani kwa kutumia usafiri wa baiskeli kwa lengo la kuhamasisha uhifadhi na utunzaji wa mazingira kwa wananchi.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo Mkuu wa wilaya ya Kasulu Luten Kanali Joseph Murimi amewataka wananchi wa Kasulu kupanda miti kwa kuwa jukumu hilo lipo katika dira ya taifa ya 2050 katika kuimarisha mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya mji Kasulu Nurfus Aziz Ndee amesema kuwa ziara hiyo itakuwa na manufaa makubwa kwa Taifa katika kuimarisha matumizi ya nishati safi, utunzaji wa mazingira na upandaji miti ili kukabiliana na mabadiliko ya TabiaNchi.
Nae Mwalimu Wenseleslaus Justine Lugaya amesema lengo la safari hiyo ni kuhamasisha wananchi kutunza maziringa na upandaji wa miti kwa ujumla ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kama Dira ya Taifa ya maendeleo ya 2050 inavyoeleza.

Safari yake itakuwa ya kilometa Elfu 8721 kwa kutumia usafiri wa baiskeli ambapo atazunguka mikoa 21 kwa Tanzania bara na Visiwani mikoa 5 na safari hiyo itaanza November 16 na kutamatika Februali 16, 2027 kwa lengo la kuhamasisha upandaji miti wa milioni 1 laki 5 na Elfu 20 kwa Taifa zima.