Buha FM Radio

Mama mjawazito hapaswi kutumia Ultrasound bila sababu za kitaalamu.

31 October 2026, 1:41 am

Mtaalamu wa maswala ya uzazi Dkt. Ally Msafiri kutoka hosptali ya Mlimani wilayani Kasulu. Picha na Irene Charles.

Kipimo vya Ultrasound kwa mama mjamzito kimekuwa na faida kubwa kwa mama na mtoto ikiwa ni pamoja na kutambua maendeleo ya ukuwaji wa mtoto akiwa tumboni na utambuzi wa magonjwa mbalimbali, lakini licha ya kuwa na faida hizo bado kinaweza kuwa na madhara kwa mama na mtoto iwapo kisipotumiwa ipasavyo.

Na Irene Charles.

Kipimo cha picha kwa kutumia mawimbi ya sauti (Ultrasound) kinaelezwa kuwa na faida ya kukadiria umri wa ujauzito, ukujua na idadi ya watoto, kutathimini ukuaji wa mtoto na kutambua matatizo ya mtoto kabla ajazaliwa.

Akizungumza na Buha FM Radio, mtaalamu wa maswala ya uzazi Dkt. Ally Msafiri Kutoka Hosptali ya Mlimani wilayani Kasulu amesema kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani WHO linapendekeza angalau Ultrasound kufanyika mara moja kabla ya wiki 24 ili kubaini mambo mbalimbali kuhusiana na ujauzito.

Sauti ya Mtaalamu wa maswala ya uzazi Dkt. Ally Msafiri kutoka hosptali ya Mlimani wilayani Kasulu.

Aidha Dkt Ally amesema Ultrasound inauwezo wa kugundua magonjwa kwa mtoto kama kichwa maji, kasoro za moyo, figo, ingawa pia haiwezi kugundua kila tatizo.

Sauti ya Mtaalamu wa maswala ya uzazi Dkt. Ally Msafiri kutoka hosptali ya Mlimani wilayani Kasulu.
Mtaalamu wa maswala ya uzazi Dkt. Ally Msafiri kutoka hosptali ya Mlimani wilayani Kasulu. Picha na Irene Charles.

Licha ya faida na ugunduzi wa baadhi ya magonjwa kwa mtoto lakini kipimo hicho pia kinatajwa kuwa na madhara kwa mama mjamzito endepo kitatumika bila kuwa na sababu za kitabibu na kushauri wajawazito kutumia kipimo hicho pale kunapokuwa na ulazima

Sauti ya Mtaalamu wa maswala ya uzazi Dkt. Ally Msafiri kutoka hosptali ya Mlimani wilayani Kasulu.

Dkt Ally ameisihi jamii kuacha kusambaza taarifa potufu kuwa kipimo hicho kusababisha ulemavu kwa mtoto aliye tumboni na kushauri watu wa karibu na mama mjamzito kuambatana kuhudhuria kliniki na kupata lishe bora.

Mfano wa picha iliyochukuliwa na kipimo cha Ultrasound kwa kuangalia maendeleo ya ujauzito. Picha na Mtandao.