Buha FM Radio

Wilaya Kasulu yatenga milioni 89.5 kukabiliana na El Niño

1 October 2026, 1:29 pm

Katibu Tawala Wilaya ya Kasulu Bi.Theresia Mtewele, akitoa maelekezo kwa watendaji wa kata zote kuhusu usafi wa mazingira. Picha na Sharifat Shinji.

Halmashauri za Wilaya ya Kasulu zimejiandaa kukabiliana na athari za mvua za El Niño zilizotangazwa na Mmlaka ya Hali ya Hewa Tanzania TMA kuwa zitaanza kunyesha hivi karibuni.

Na; Sharifat Shinji

Wilaya ya Kasulu kupitia Halmashauri zake imejiandaa kukabiliana na athari za mvua za El Niño zinazotarajiwa kunyesha siku za karibuni ambapo Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Bi.Theresia Mtewele, amewaelekeza watendaji wa kata wote kuhakikisha Jumamosi ya Oktoba 3, 2026 inatumika kuwa siku maalum ya usafi katika maeneo yao ya kazi.

Theresia ametoa agizo hilo wakati wa kikao cha dharura cha Kamati ya Usimamizi wa Maafa ya Wilaya kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji Kasulu, akiwataka watendaji kuhakikisha mifereji inazibuliwa, wananchi wanaoishi mabondeni na maeneo mengine hatarishi wanafuatiliwa na hatua stahiki zinachukuliwa kwa mujibu wa taratibu.

Sauti ya Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Bi.Theresia Mtewele.

Kwa upande wake Mratibu wa Maafa Halmashauri ya Mji Kasulu Mchumi Edwini Lauliani amesema Halmashauri imetenga jumla ya milioni 11.5 kwa ajili ya dharura ya mvua hizo na tayari wameanza kutoa elimu kwa wananchi namna ya kukabiliana na mvua hizo pamoja na kufanya usafi katika mifereji ya maji.

Sauti ya Mchumi Edwini Lauliani.

Nae Mchumi Fadhili Ndunguru ambaye ni Mratibu wa Maafa Halimashauri ya Wilaya ya Kasulu amesema jumla ya milioni 78 imetengwa kusaidia maeneo hatarishi katika kata zaidi ya nane  ambapo pesa hiyo itatumika kwa mgawanyo wa kabula ya madhra ya mvua na baada ya  madhara ya mvua hizo.

Sauti ya Mchumi Fadhili Ndunguru.

Halmashauri zote mbili zimetenga jumla ya Milioni 89.5 kwa ajili ya kukabiliana na madhara yote yanayoweza kujitokeza ndani ya Halmashauri hizo ambapo Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania TMA, ilitangaza Mvua za El Nino zinatarajiwa kuanza kunyesha mwezi October na kuendelea hivyo wananchi wanatakiwa kuchukua taadhari za mapea kabla na baada ya mvua hizo.