Buha FM Radio
Buha FM Radio
7 November 2026, 1:45 am

Licha serikali kuanzisha mpango na utaratibu wa wanafunzi kupata chakula shuleni wakati wa masomo kwa lengo la kupunguza utoro na kuongeza ufaulu katika shule mbalimbali nchini lakini imeelezwa kuwa chakula wanachopewa baadhi ya wanafunzi hao hakina virutubisho muhimu vinavyotakiwa jambo linalorudisha nyuma jitihada za kikabiliana na utapiamlo na ukosefu wa lishe.
Na; Paulina Majaliwa
Wazabuni wanaosambaza vyakula katika shule mbalimbali mkoani Kigoma wametakiwa kuongeza virutubisho katika vyakula hivyo kwa ajili ya kuongeza lishe kwa wanafunzi.
Hayo yamesema na Afisa mwandamizi kutoka Wizara ya afya Peter Francis Kaja wakati akitoa semina kwa wazabuni, pamoja na baadhi ya watumishi wa afya juu ya sera na kanuni za urutubishaji vyakula ili kukabiliana na tatizo la utapiamlo na upungufu wa madini na vitamini nchini.

Aidha amewataka maafisa afya pamoja na mafisa lishe kwa kushirikiana na maafisa afya ngazi za mtaa, kijiji mpaka kata mkoani Kigoma kuendeelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya kuimarisha lishe ngazi ya kaya na jamii kwa ujumla
Kwa upande wake afisa lishe wa mkoa wa Kigoma James Ngalaba amesema baadhi ya wazabuni wamekuwa wakisambaza unga usiokuwa na virutubishi na kusema serikali mkoani humo itaanzisha sera ya kukagua vyakula shuleni na kununua mashine za urutubishaji lengo ni kuimarisha lishe kwa wanafunzi hao.
Sauti ya Afisa lishe wa mkoa wa Kigoma James Ngalaba
Katika hatua nyingine amewasisitiza wazabuni, maafisa lishe na maafisa afya kutoka mkoani Kigoma kuendelea kuzitambua na kuzitumia mashine za urutubishaji huku akisema mashine hizo zitaendelea kuongezwa kila wilaya.
Wizara ya afya, Wizara ya Viwanda na Biashara na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wazabuni au wasambazaji wa chakula shuleni wanajukumu la kuhakikisha chakula kinachofika kwa wanafunzi kiko salama, bora na kinazingatia viwango vinavyotakiwa vya lishe.