Buha FM Radio

Haki ya elimu kwa watoto wenye ulemavu imetekelezwa?

23 November 2026, 7:40 pm

Watoto wenye ulemavu wakiwa shuleni wakiendelea na masomo. Picha kwa mujibu wa akili unde (chatgtp).

Kutokana na takwimu mbalimbali ikiwemo takwimu za Ofisi ya Taifa ya Takwimu nchini Tanzania NBS za Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, baadhi ya watu wenye ulemavu hawajawahi kupata fursa ya kwenda shule.

Imeandikwa na Sharifat Shinji na Kusimuliwa na Ramadhan Zaidy

Kwa mujibu wa Ripoti ya Haki za Binadamu ya mwaka 2023 iliyotolewa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), asilimia 48 ya washiriki wa utafiti walitaja unyanyapaa na ubaguzi kuwa miongoni mwa changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu, huku asilimia 28 wakitaja upatikanaji mdogo wa elimu bora.

Takwimu hizo zinaibua hoja kuhusu namna jamii inavyowatendea watoto wenye ulemavu na mchango wake katika kuhakikisha wanapata fursa sawa za elimu, Buha FM radio imeandaa makala inayohusu “Haki ya elimu kwa watoto wenye ulemavu imetekelezwa?”.