Radio Kwizera
Radio Kwizera
October 12, 2026, 1:24 pm

Wakulima wamebainisha kuwa fursa hiyo imewezesha kuinuka uchumi huku wakiwataka vijana kuchangamkia fursa hiyo.
Na Samwel Masunzu- Kibondo, KIGOMA
Baadhi ya wakazi wa kijiji na kata ya Kumwambu wilayani Kibondo mkoani Kigoma wamegeuza uoteshaji miti kuwa fursa ya kiuchumi.
Wakizungumza na Radio Kwizera baadhi yao Bw. Emily Magambo, Keneth Isaka na Tumaini Magambo wamesema fursa hiyo imewezesha kuinua uchumi huku wakilitaka kundi la vijana kuichangamkia.
Wamesema licha ya baadhi ya miche kuuzwa kwa bei shilingi 100 na mingine 1,000 hadi 3,000 lakini vijana wanaweza kuitumia katika kuinua uchumi badala ya kulalamikia kukosa shughuli za kufanya.

Aidha wameomba wadau mbalimbali kuendelea kuunga mkono jitihada hizo ambazo huwezesha katika utunzaji wa mazingira.