Radio Kwizera
Radio Kwizera
May 15, 2026, 12:50 pm

Tukio hilo lilitokea Mei 12 mwaka huu kijiji cha Nyarututu Kata ya Bwanga Wilayani Chato ambapo marehemu alikutwa amefariki nyumbani katika mazingira ambayo Jeshi hilo limebaini ni yakughushi.
Na Clement Shawishi – GEITA
Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia kwa mahojiano zaidi Mchungaji wa Kanisa la Habari Njema Bw. Basese Gervas Bilalo kwa tuhuma za mauaji ya mke wake Bi. Martha Faustine.
Kamanda wa Polisi Mkoani humo Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Safia Jongo amesema hayo na kwamba uchunguzi wa awali umebaini mtuhumiwa alimkaba marehemu kwa kamba ya katani.
Kupitia taarifa hiyo, Kamanda Jongo amesema tukio hilo lilitokea Mei 12 mwaka huu kijiji cha Nyarututu Kata ya Bwanga Wilayani Chato ambapo marehemu alikutwa amefariki nyumbani katika mazingira ambayo Jeshi hilo limebaini ni yakughushi.
Chanzo cha tukio kinadaiwa kuwa migogoro ya kifamilia kupitia marehemu kumtuhumu Mumewe kuwa na mahusiano nje ya ndoa, Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Wilaya ya Chato kwa uchunguzi na taratibu nyingine za kisheria zinaendelea.