Radio Kwizera

ACT Wazalendo wapinga matokeo uchaguzi jimbo la Mbarali, kukata rufaa mahakamani

September 21, 2023, 1:50 pm

Katibu Mkuu wa chama cha ACT Wazalendo Ndugu Ado Shaibu.

Chama cha ACT Wazalendo kimesema hakikubaliani na matokeo ya Ubunge yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na kutangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mbarali Ndugu Missana K. Kwangura Septemba20,2023.

Na Laurent Gervas:

Chama cha ACT Wazalendo chapinga matokeo ya uchaguzi mdogo Jimbo la Mbarali cha sema kinapanga kukata rufaa mahakamani.

Chama cha ACT Wazalendo kimesema hakikubaliani na matokeo ya Ubunge yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na kutangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mbarali Ndugu Missana K. Kwangura Septemba20,2023.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa chama cha ACT Wazalendo Ndugu Ado Shaibu wakati akizungumza na Radio kwizera ilipotaka kujua tathimini ya uchaguzi kwa chama hicho.

Amesema Uchaguzi ulikuwa na kasoro nyingi sana ikiwemo, Msimamizi wa Uchaguzi kuvuruga zoezi la kuapisha mawakala ambapo maeneo ambayo aliahidi kuapisha mchana alifika usiku.

Nakala ya matokeo ya uchaguzi wa Ubunge jimbo la Mbarali.

Amesema hali hiyo ilisababisha baadhi ya Mawakala wao na wa vyama vingine wasiapishwe ambapo hata CCM iliyoapisha mawakala wachache sana kuliko ACT Wazalendo Cha kustaajabisha, asubuhi ya siku ya kupiga kura, CCM ilikuwa na mawakala katika vituo vyote.

Ndugu Ado amesema CCM ilitumia vituo ambavyo mawakala wa ACT Wazalendo walizuiwa, kuweka matokeo ya uongo.

Katika uchaguzi huo Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Mbarali Missana K. Kwangura alimtangaza Ndugu Bahati Keneth Ndingo kuwa mshindi baada ya kupata kura 44334 dhidi ya kura 10014 za Modestus Kirufi wa ACT Wazalendo.

Hata hivyo Radio Kwizera fm imemtafuta kwa simu Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Mbarali Missana K. Kwangura ambapo simu imeita mara kadhaa bila kupokelewa.