Radio Kwizera

Biteko amtaka Aweso kufanya ziara kata ya Murusagamba

September 29, 2023, 9:39 pm

Naibu waziri mkuu na waziri wa wizara ya Nishati Dr.Dotto Mashaka Biteko akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ntanga Kata ya Murusagamba wilayani Ngara mkoani Kagera.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dr.Dotto Mashaka Biteko amemtaka Waziri wa Maji Juma Aweso kufanya ziara katika kata ya Murusagamba wilayani Ngara ili kutatua changamoto ya maji kwa wananchi hao.

Na, Marco Pastory:

Naibu Waziri Mkuu ameyasema hayo leo katika ziara anayoendelea kuifanya wilayani Ngara kwa lengo la kuzindua umeme vijijini awamu ya tatu na kuzungumza na wananchi ili kutatua changamoto walizonazo.

Akizungumza kwa njia ya simu na Dkt Biteko kwenye mkutano huo, Waziri wa Maji Juma Aweso amesema, wiki ijayo atafanya ziara kwenye maeneo hayo ili kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji

Awali akieleza changamoto ya maji kwenye kata ya Murusagamba Mbunge wa Jimbo la Ngara Bw Ndaisaba Ruhoro amesema wananchi wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya upatikani wa maji jambo linalorudisha nyuma maendeleo yao.