Radio Kwizera

Serikali yashauriwa kufufua Vivutio vya Utalii ili kukuza Uchumi

April 28, 2026, 11:54 am

Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Utalii Kagera wakiwa na Viongozi wao walipotembelea maporomoko ya mto Kisuma yaliyopo kijiji cha Katerela, kata ya Ruziba, Biharamulo. Picha na William Mpanju

Mkurugenzi wa Chuo cha Utalii Kagera kilichopo Biharamulo, Bw. Stanley Thomas amesema uwekezaji katika vivutio hivyo unaweza kusaidia kuongeza mapato ya ndani pamoja na fedha za kigeni

Na William Mpanju- Biharamulo, KAGERA

Serikali imeshauriwa kuchukua hatua za makusudi katika kufufua vivutio vya utalii vilivyopo kwenye halmashauri mbalimbali ili kuongeza mchango wake katika uchumi wa taifa.

Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi wa Chuo cha Utalii Kagera kilichopo Biharamulo, Bw. Stanley Thomas, wakati wa ziara ya wanafunzi waliotembelea maporomoko ya mto Kisuma yaliyopo kijiji cha Katerela, kata ya Ruziba.

Amesema uwekezaji katika vivutio hivyo unaweza kusaidia kuongeza mapato ya ndani pamoja na fedha za kigeni, lakini bado kuna changamoto za miundombinu na uendelezaji.