Radio Kwizera

Ngara yatoa mwelekeo mpya wa kuuenzi Muungano

April 28, 2026, 1:37 pm

Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Kanal Mathias Kahabi (aliyepiga magoti) akishiriki zoezi la kupanda miti wilayani Ngara mkoani Kagera. Picha na David Mwaluseke

Shughuli zilizofanyika ni pamoja na usafi wa mazingira, mazoezi na upandaji miti katika Shule ya Msingi Ngara Mjini, ikiwa ni sehemu ya kuenzi na kuendeleza mshikamano miongoni mwa wananchi.

Na David Mwaluseke- Ngara, KAGERA

Baada ya maadhimisho ya miaka 62 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kufanyika jana, Halmashauri ya Wilaya ya Ngara mkoani Kagera imeendelea kusisitiza umuhimu wa kudumisha tunu za muungano kupitia shughuli mbalimbali za kijamii.

Shughuli zilizofanyika ni pamoja na usafi wa mazingira, mazoezi na upandaji miti katika Shule ya Msingi Ngara Mjini, ikiwa ni sehemu ya kuenzi na kuendeleza mshikamano miongoni mwa wananchi.

Akizungumza wakati wa kuhitimisha kongamano lililoambatana na maadhimisho hayo, Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Kanal Mathias Kahabi, amesema muungano ni tunu muhimu ya taifa inayopaswa kulindwa na kuendelezwa kwa vitendo kila siku.

Aidha, amewataka wananchi wa wilaya hiyo kuendelea kuwahamasisha wageni wanaoingia kutoka nchi jirani kufuata taratibu rasmi ili kudumisha usalama na utulivu wa eneo hilo.

Maadhimisho ya mwaka huu yaliongozwa na kaulimbiu isemayo “Miaka 62 ya Muungano: Amani, Umoja na Mashikamano ni Msingi wa Maendeleo Endelevu.”